Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaume anayegombea kiti cha uongozi cha wanawake

 121475527 Whatsappimage2021 11 08at8 Mwanaume anayegombea kiti cha uongozi cha wanawake

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: BBC

Ameer Sarkee, mwanaume kutoka nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 26, ambaye anagombea kiti maalum cha wanawake katika chama tawala cha Nigeria UPC, ameiambia BBC kuwa anagombea kiti hicho kwasababu yeye ni mwanaume ambaye anapaswa kusimamia mausla ya wanawake wakati wote.

Mwaka 2019 Bw Ameer aligombea kiti cha wanawake kupitia chama cha PDP tawi la la Kano lakini hakuweza kuchaguliwa. Laini ansema mara hii hatakubali kushindwa kwasababu lazima ashugulikie masuala ya wanawake.

"Tangu nilipokuwa mtoto nilikuwa nikiwaona wanawake wanaohitaji msaada na kuwasaidia-kama vile kubeba nguo au kuwanunulia kitu fulani-na ndio maana ninataka kuwa kiongozi wa wanawake katika chama chetu ," alisema.

"Baadhi ya watu huniuliza kwanini unagombea uenyekiti wa wanawake na jibu langu ni ‘Mungu aliumba mwanaume awapende wanawake ,'" alisema Ameer.

Chanzo: BBC