Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasiasa wa upinzani Eswatini auawa kwa kupigwa risasi

Auawa Eswatiniiiiiiiiiiiiiiii.png Mwanasiasa wa upinzani Eswatini auawa kwa kupigwa risasi

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wenye silaha nchini Eswatini wamemuua kwa kumpiga risasi mwanasiasa mashuhuri wa upinzani na ambaye pia alikuwa mwanasheria wa haki za binadamu.

Hayo yameelezwa na msemaji wa chama chake ambaye ameziambia duru za habari, saa chache baada ya mfalme wa nchi hiyo kuwashutumu wanaharakati wanaopinga utawala wake.

Thulani Maseko aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake Jumamosi usiku na washambuliaji wasiojulikana huko Luhleko, yapata kilomita 50 kutoka mji mkuu Mbabane, msemaji wa chama cha upinzani Sikelela Dlamini amesema.

Msemaji huyo amesema aliambiwa “wauaji walimpiga risasi kupitia dirisha akiwa ndani ya nyumba na familia yake”.

Serikali ilituma salamu za rambirambi kwa familia yake, ikisema kifo cha Maseko ni “hasara kwa taifa” na kwamba polisi wameanzisha msako dhidi ya waliohuusika na mauaji hayo.

Maseko alikuwa mwanasheria kiongozi wa haki za binadamu na mwandishi wa maoni nchini Eswatini, ambaye alikuwa na kesi inayoendelea mahakamani dhidi ya uamuzi wa Mfalme Mswati wa tatu kubadili jina la nchi na kuipa jina la Eswatini kwa amri.

Jina la nchi lilibadilishwa kutoka Swaziland na kuitwa Eswatini kwa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 2018.

Msimamo wa mwanasiasa huyo wa upinzani ulikuwa kwamba Mfalme hakufuata utaratibu wa katiba.

Kuuawa masaa machache mpinzani huyo baada ya mfalme wa nchi hiyo kuwashutumu wanaharakati wanaopinga utawala wake, kumezua maswali mengi yasiyo na majibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live