Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasiasa wa UDA Francis Mureithi akamatwa akiwa nyumbani kwake

0fgjhs635jde1t4j4 Mwanasiasa wa UDA Francis Mureithi akamatwa akiwa nyumbani kwake

Fri, 23 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Francis Mureithi ameripotiwa kukamatwa usiku wa kuamkia Alhamisi, Julai 22 akiwa nyumbani kwake NairobiPolisi waliomkamata hawakupeana taarifa kamilifu lakini inadaiwa mwanasiasa huyo alihusishwa na ajali kule magharibi mwa KenyaImeripotiwa kwamba Mureithi amesafirishwa hadi mkoa wa magharibi ambapo anatarajiwa kufikishwa katika mahakama mojaMureithi alikuwa mgombea wa kiti cha ubunge cha Embakasi Mashariki katika uchaguzi mkuu wa 2017Aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge cha Embakasi Mashariki Francis Mureithi alikamatwa mapema siku ya Alhamisi, Julai 22 akiwa nyumbani kwake Nairobi.

Mureirthi ambaye ni mwandani wa karibu wa Naibu Rais William Ruto na mwanachama wa chama cha UDA, anadaiwa kusababisha ajali kule mkoani magharibi lakini polisi waliomkamata hawakupeana taarifa kamilifu

Akizungumza na wanahabari, mwakilishi wa mawasiliano wa chama cha UDA Wanjohi Githae alithibitisha kwamba mwanasiasa huyo amesafirishwa eneo la magharibi ambapo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu kesi dhidi yake.



Read also

Ruto Apokonya Uhuru 'Mali' Yake na Habari Zingine za Kusisimua Wiki Hii

Kulingana na baadhi ya wafuasi wake, kesi hiyo ilikuwa imetatuliwa kwa amani na waliohusika kwenye ajali na wanashangaa tena iweje ilipelekwa kortini.

" Alikamatwa akiwa nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo, anakabiliwa na kesi ambayo inahusiana na ajali, tuko hapa kumshughulikia," Alisema Githae.

" Atafikishwa katika mahakama moja ya magharibi mwa Kenya lakini polisi hawajatupea taarifa kamilifu. Mawakili wetu wanajaribu kufuatilia waone jinsi mambo yanavyoendelea," Aliongezea Githae.

Mureithi alipoteza kiti cha eneo bunge la Embakasi Mashariki kwa Babu Owino baada ya mahakama kuridhisha ushindi wa Owino katika uchaguzi wa 2017.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke