Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasiasa 'awapokonya' wananchi gari la wagonjwa baada kushindwa uchaguzi

Mwanasiasa Aliyeshindwa Uchaguzi Na Kuchukua Ambulensi Mwanasiasa 'awapokonya' wananchi gari la wagonjwa baada kushindwa uchaguzi

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mwanasiasa wa Uganda Evelyn Anite Jumanne alijibu baada ya akaunti ya Twitter kufufua kumbukumbu ya tukio la kushangaza lililomhusisha takriban miaka miwili iliyopita.

Akaunti ya Twitter @AfricaFactsZone ilikuwa imechapisha kumbukumbu kutoka mwaka wa 2021 wakati mwanasiasa huyo alipochukua gari la wagonjwa alilokuwa ametoa kwa wakazi wa Manispaa ya Kaboko ambapo alikuwa akiwania kiti cha ubunge.

Bi Anite ambaye alishindwa katika uchaguzi mkuu wa Septemba 2020 alikuwa ametoa ambulensi ili kuwezesha usafirishaji wa akina mama hospitalini ili kusaidia kupunguza vifo vya wajawazito na wanaojifungulia nyumbani.

"Mwanasiasa wa Uganda, Evelyn Anite alichukua tena gari la wagonjwa alilokuwa ametoa kwa wilaya yake, baada ya kushindwa katika uchaguzi wa 2021," @AfricaFactsZone iliandika.

Akijibu chapisho hilo, Bi Anite alithibitisha kuwa ni kweli alichukua gari hilo na kubainisha kwamba hana majuto yoyote.

Alisema alichukua hatua hiyo kwa kuwa wakazi hawakumpigia kura licha ya kuwaonyesha sababu za kumchagua k.v kuwapa gari la wagonjwa.

“Asante kwa kuleta hili. Kwanza, ni kweli nilichukua gari langu la wagonjwa na sijaomba msamaha kwa hilo. Kwa nini nilifanya hivyo? Ni kwa sababu hawakunipigia kura.Kwa hiyo ulitarajia niondoke bila chochote?,” Anite alisema na kunukuu mstari wa Biblia kutoka Wagalatia 6:7 unaozungumza kuhusu mtu kuvuna alichopanda.

Alipoambiwa kwamba hana aibu juu ya kitendo chake, alisema, "Kama wapiga kura, kwa nini ungekosa kumchagua mtu ambaye amekupa gari la wagonjwa?"

Anite alikiri kwamba aliumia sana baada ya wakazi wa Manispaa ya Kaboko kumnyima kura licha ya kujaribu kuwavutia kwa gari la wagonjwa.

"Kutonipa kura ilikuwa rushwa," alisema.

Mwanasiasa huyo alithibitisha kwa ujasiri kwamba aliuza ambulensi baada ya kuirudisha kutoka kwa jamii.

Chanzo: Radio Jambo