Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasiasa Zimbabwe ahukumiwa kwa ujumbe wa uwongo Twitter

Mwanasiasa Zimbabwe Ahukumiwa Kwa Ujumbe Wa Uwongo Twitter Mwanasiasa Zimbabwe ahukumiwa kwa ujumbe wa uwongo Twitter

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mwanasiasa mmoja wa upinzani nchini Zimbabwe, Fadzayi Mahere, amepatikana na hatia ya kusambaza uongo kwa kutuma tena video ya mwaka 2021 akidai kuwa afisa wa trafiki alimuua mtoto mchanga.

Ilibainika kuwa mtoto huyo alikuwa hai, na hakuwa amepata majeraha yoyote.

Hakimu Taurai Manwere alisema ujumbe wake wa Twitter ulikuwa uzembe, na ililenga kudhoofisha imani ya umma kwa polisi.Hakimu alisema alipaswa kwanza kuthibitisha habari hizo.

Bado hajahukumiwa.

Chama cha Bi Mahere - Citzens' Coalition for Change (CCC) kimelaani hukumu hiyo.

"Anateswa kwa msimamo wake wa kisiasa," ilisema.

Chanzo: Bbc