Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasheria atabiri Afrika Kusini kushinda madai dhidi ya Israel

Afrika Kusini Kusini Mwanasheria atabiri Afrika Kusini kushinda madai dhidi ya Israel

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afrika Kusini ina ushahidi imara na ‘itashinda kesi ya yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ya kuilazimu Isitishe mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina’

Hayo ni kwa mujibu wa mwanasheria wa kimataifa wa haki za binadamu Francis Boyle anayesifika kwa mafanikio yake katika kesi za mauaji ya kimbari katika ya Umoja wa Mataifa ya ICJ. Amesema anaona uwezekano mkubwa wa Afrika Kusini kushinda kesi yake dhidi ya Israel.

ICJ, mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa inayojulikana pia kama Mahakama ya Dunia, itaanza kusikilizwa Alhamisi hii mjini The Hague kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini ikiishutumu Israel kwa kutekeleza mauaji ya kimbari, kinyume na Mkataba wa Mauaji ya Kimbari wa mwaka 1948.

Mkataba huo unafafanua mauaji ya halaiki au kimbari kuwa “vitendo vinavyofanywa kwa nia ya kuharibu, kwa ujumla au kwa sehemu, kikundi cha kitaifa, kikabila, cha rangi au cha kidini.”

Kesi hiyo yenye kurasa 84 pia inaitaka ICJ kuchukua hatua za haraka za kuishurutisha Israel kukomesha l uhalifu zaidi huko Gaza, ambako mashambulizi yake tangu Oktoba 7 hadi yameua zaidi ya raia 23,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Mwanasheria wa kimataifa wa haki za binadamu Francis Boyle alisema katika mahojiano ya video na Shirika la Habari la AA amesema, "Nimesoma maombi yote ya Afrika Kusini ... na uchambuzi wangu, kulingana na ujuzi na uzoefu wangu, ni kwamba Afrika Kusini itashinda kesi dhidi ya utawala wa Israel na utawala huo utalazimishwa kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.” Hali baada ya utawala katili wa Israel kudondosha mabomu katika makazi ya raia Ukanda wa Gaza

Boyle, ambaye alishinda maombi mawili katika ICJ mwaka 1993 chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari alipoiwakilisha Jamhuri ya Bosnia na Herzegovina dhidi ya Yugoslavia, alisema Afrika Kusini ina timu ya "mawakili wa kimataifa wa kiwango cha juu" katika kesi hiyo.

Agizo kama hilo "linaweza kuwa na athari mbaya kwa Israel," alisema Boyle, alipokuwa akielezea hali mbalimbali, kuanzia Afrika Kusini kwenda katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kwa ajili ya kutekeleza amri ya uwezekano wa kusimamishwa kwa Israel kuwa mwanachama wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na hata uwezekano wa vikwazo vya kiuchumi.

Alisema, "Wakati huo, dunia nzima itajua kwamba Israel inatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina,"

Aidha amesema iwapo Afrika Kusini itafaulu katika ICJ Afrika Kusini itafikishe faili hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya utekelezaji, ambapo inaweza kukabiliana na vikwazo, hasa kutoka kwa washirika wenye nguvu wa utawala haramu wa Isarel

Kuhusu uamuzi wa Israel wa kupinga kesi hiyo, wakili huyo alisema unatokana na imani kwamba “Amri ya Mahakama ya Ulimwengu dhidi yake itakuwa pigo kubwa ambalo litaidhuru daima.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live