Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasheria Mkuu apinga kauli ya Chebukati kulazimishwa kutangaza matokeo

Paul Kihara Kariuki.jpeg Mwanasheria Mkuu apinga kauli ya Chebukati kulazimishwa kutangaza matokeo

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Paul Kihara Kariuki amepinga madai ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEBC), Wafula Chebukati kuwa Maafisa Wakuu Serikalini ambao ni Wajumbe wa Baraza la Usalama la Taifa walijaribu kumshinikiza kutomtangaza William Ruto kuwa Rais Mteule.

Mwanasheria Mkuu pia aliitaka Mahakama Kuu kufafanua masharti ya Ibara ya 138 ya Katiba kuhusu (Utaratibu wa Uchaguzi wa Rais) na majukumu ya Mwenyekiti wa Tume pamoja na nafasi ya Tume kama chombo katika uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais.

Kutokana na mgogoro ulioibuka baina ya Makamishna waliokataa Matokeo ya Urais na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, Mahakama Kuu imeombwa kuweka wazi jukumu la Makamishna wote wa Tume katika Kujumlisha, Kuhakiki na Kutangaza Matokeo ya Uchaguzi ya Urais ili kuepusha mizozo katika chaguzi zijazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live