Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanariadha nguli Kenya kuzikwa Ijumaa

Aa9fe0f6989f042550ed5c2b1cc2a820 Mwanariadha nguli Kenya kuzikwa Ijumaa

Tue, 28 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BINGWA wa medali ya fedha ya Olimpiki 1968 wa mbio za meta 1,500 Ben Jipcho, aliyefariki dunia wiki iliyopita, atazikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Kisawai Ijumaa, imeelezwa.

Kwa mujibu wa mtoto wake wa kiume, David Kwenden, baada ya majadilioano marefu na viongozi wa serikali na wadau wa mchezo wa riadha wamekubaliana maziko hayo kufanyika Ijumaa.

“Tulikuwa na majadiliano marefu na serilali na viongozi wa Riadha Kenya na tumekubaliana kuwa maziko yatafanyika Ijumaa. Jumatano tutaangalia gharama za maziko, “alisema Kwenden.

Alisema kuwa baba yake alikuwa mtu mkubwa mwenye kuheshimiwa duniani na wanaimani watamuaga vizuri.

“Ni bahati mbaya katika kipindi hiki kuna janga la Covid-19 ambako kuna miongozi imetolewa kwa ajili ya mazishi. Tunapanga kumuaga vizuri kwa sababu alikuwa alama na amekuwa akiheshimika dunia nzima katika riadha, “alisema mtoto wake huyo.

Rais wa Riadha Kenya alisema kuwa shirikisho hilo la riadha liko pamoja na familia ya marehemu.

"Maandalizi ya mazishi ya Jipcho yanaendelea vizuri na sisi kama shirikisho tunaisaidia familia. Jipcho alikuwa alama na anatakiwa kupewa heshima yake kwa kuagwa vizuri, “alisema Tuwei.

Wengi wanamkunbuka mwanariadha hiyo kama mfannyakazi hodari ambaye wakati wote alikuwa akifanya mambio mazuri hasa wakati ule akishiriki riadha.

Kipchoge Keino ambaye alifanya mazoezi na kushindana pamoja katika mashindano mbalimbali duniani alisema kuwa alikuwa hodari na mwenyekujua jinsi ya kupata medali.

“Tulikuwa tunashiriiana na Jipcho na tunajua jinsi ya kupata mjedali wakati fulani katika Michezo ya Olimpiki ya Mexico 1968, alinisaidia mimi kupata medali yangu ya kwanza ya dhahabu katika mbio za meta 1,500. Tunaomboleza kifo cha shujaa na tuko pamoja na familia yake katika kipindi hiki, “alisema Kipchoge.

Jipcho, ambaye alianza riadha katika miaka ya 1960, atakumbukwa kuwa mmoja wa `wasindikizaji’ wa kwanza wasio rasmi baada ya kujitolea nafasi yake ya kushinda medali ili mwenzake Kipchoge Keino ashinde dhahabu katika mbio za meta 1,500 wakati wa Michezo ya Olimpiki 1968 na yeye alimaliza wa 10.

Mwaka 1970, Jipcho alishinda medali ya fedha katika meta 3,000 kuruka gogo na maji katika Michezo ya Jumuiya ya Madola huko Edinburg kabla hajapata medali ya fedha katika Michezo ya Olimpiki huko Munich mwaka 1972 ambako pia alishiriki meta 3,000 kuruka viunzi na maji.

Mwaka 1973, alishiriki katika Michezo ya Mataifa ya Afrika Lagos, Nigeria ambako alishiriki mbio mbili, na kupata medali za dhahabu katika meta 5,000 na ile ya 3,000 kuruka viunzi na maji.

Mwaka 1974, alitwaa meali za dhahabu katika meta 5,000 na 3,000 kuruka viunzi na maji na mbio za meta 1,500 alipata medali ya shaba wakati wa Michezo ya Jumuiya ya Madola huko Christchurch, New Zealand.

Katika michezo hiyo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka 1974, Mtanzania Filbert Bayi alitwaa medali ya dhahabu yam bio za meta 1,500 na kuweka rekodi ya dunia iliyodumu kwa takribani miaka mitano kabla ya kuvunjwa na Muingereza Sebastian Coe.

Chanzo: habarileo.co.tz