Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamume amuua mwenzake kwa kutomlipa deni

Unnamed (1).png Mwanamume amuua mwenzake kwa kutomlipa deni

Fri, 4 Aug 2023 Chanzo: Radio Jambo

Wanaume wawili wa umri wa makamo walipoteza maisha yao Alhamisi huko Lokichar, Kaunti ya Turkana, kufuatia visa viwili vinavyohusiana vilivyohusishwa na deni ambalo halijalipwa.

Mmoja wa waathiriwa anasemekana kumdunga kisu mwingine kifuani kwa kukosa kulipa deni la Ksh.50 lililoripotiwa kupatikana kutokana na mauzo ya kuku.

Mtu aliyechomwa kisu alifariki mara baada ya tukio hilo, huku muhusika akikimbia baada ya kundi la watu kuanza kukusanyika eneo la tukio

Juhudi zake ziliambulia patupu kwani umati huo wenye hasira ulimkamata na kumpiga mawe hadi kufa.

"Alijaribu kutoroka lakini umati wenye hasira ulimfuata na kumpata. Kisha wakampiga kwa mawe hadi kufa," shahidi aliyeshuhudia aliambia runinga ya Citizen.

Miili ya wawili hao imehamishiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Lodwar.

Wazee wa eneo hilo wamelaani kisa hicho huku wakiwataka vijana kutosababisha vurugu wakati wa kusuluhisha tofauti zao.

Chanzo: Radio Jambo