Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamume amuua mama’ke kisa shilingi laki moja

Ephantus Kiura Ephantus Kiura

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi katika eneo la Kirinyaga nchini Kenya wamemkamata mwanamume anayeshukiwa kumuua mamake katika kijiji cha Kiarigi huko Mwea Mashariki.

Kamanda wa Polisi eneo hilo Daniel Kitavi alisema mshukiwa, Ephantus Kiura Ndambiri alikamatwa katika kijiji cha Gacuriri huko Mbeere, Kaunti ya Embu.

Mzee huyo wa umri wa miaka 53 anasemekana kumpiga Grace Muthoni Ndambiri mwenye umri wa miaka 75 kwa kutumia kifaa mnamo Juni 12, 2022 na kumuua papo hapo.

Uchunguzi wa awali ulifichua kuwa mshukiwa alitofautiana na mamake baada ya kudaiwa kukataa ombi lake la kumpa shilingi za Ksh.6000 (sawa na Tsh 118,000).

Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Wanguru baada ya mahakama kuwapa wachunguzi muda wa wiki mbili kuchunguza kisa hicho.

Ikumbukwe kwamba hapo nyuma kulikuwa na visa vingi vya mauaji kule Kaonti ya Nakuru na walioadhiriwa sana ni wanawake, wakazi wa Nakuru sasa wanataka kujua ni nani ambaye anajihushisha na mauaji hayo kule Nakuru.

Katika kisa cha kwanza, Bi Grace Wambui, 21, alipatikana ameuawa Juni 15 nyumbani kwake. Wiki moja tu baadaye, mwanamke mwingine aliyejulikana kama Bi Susan Wambui aliuawa na mwili wake kupatikana chumbani mwake.

Takriban washukiwa 27 wametiwa Baroni katika msako unaoendelea dhidi ya genge maarufu na makundi mengine ya uhalifu katika mji wa Nakuru.

Dkt Matiang'i alitangaza oparesheni kali ya kuwanasa wanachama wa genge hilo ambalo limekuwa likifanya uharibifu mjini Nakuru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live