Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke wa miaka 25 ajifungua watoto 9 kwa mpigo, wakiume na wakike

Screenshot 2021 05 05 At 23.31.54 660x400.png Mwanamke wa miaka 25 ajifungua watoto 9 kwa mpigo, wakiume na wakike

Thu, 6 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Kuna taarifa hii kutokea nchini Morocco ambapo raia wa Mali, Halima Cisse mwenyewe miaka 25 amejifungua watoto 9 kwa mpigo wanne wakiwa wakiume na watano wakike.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Mali imebainisha kwamba Halima amejifungulia nchini Morocco baada Madaktari kushauri aende nchini humo kwa sababu kuna wabobezi wa masuala ya Uzazi.

Hatua hiyo ilitokana na kufanya vipimo ikiwemo Ultra Sound ambapo ilibainika ana watoto 7 lakini siku ya kujifungua akajifungua watoto 9 huku ikielezwa Ultra Sound ilishindwa kuona watoto wawili.

Kwa mujibu wa kitengo cha Afya nchini Morocco kimebainisha kuwa Halima na watoto wake wanaendelea vizuri na wiki kadhaa zijazo watarudi nchini kwao Mali.

Chanzo: millardayo.com