Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke raia wa Kenya akamatwa Ghana kwa kuingiza Cocaine

Mwanamke Raia Wa Kenya Akamatwa Ghana Kwa Kuingiza Cocaine Mwanamke raia wa Kenya akamatwa Ghana kwa kuingiza Cocaine

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Ghana zimesema kuwa zimemkamata mwanamke Mkenya kwa kusafirisha kilo11.0 za kokeni yenye thamani ya zaidi ya Dola Laki Tatu ($309,120) kuingia nchini humo.

Mshukiwa huyo aliyetambulika kwa jina la Njeri Mary, alikamatwa wikiendi na maafisa wa Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya (NARCOC) wakati wa ukaguzi wa kawaida katika ukumbi wa kuwasili wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka mjini Accra.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 35 alikuwa ameshuka kutoka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini kutoka Nairobi hadi Accra kupitia Johannesburg.

Inasemekana alificha dawa hizo kwenye vifurushi vya vyakula vya Cremora na alikamatwa alipokiri kumiliki mzigo huo.

Kwa sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa gerezani kwa uchunguzi zaidi ili kujua ni nani aliyemtuma na mtu aliyekuwa akileta mzigo huo nchini.

Ni kinyume cha sheria nchini Ghana kumiliki au kusafirisha dawa za kulevya. Kosa hilo linaweza kusababisha kifungo cha kati ya miaka 10 na 25 iwapo atapatikana na hatia.

Chanzo: Bbc