Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke miaka 61 aupigwa shoti ya umeme na kufariki

SHOTII.jpeg Mwanamke miaka 61 aupigwa shoti ya umeme na kufariki

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa kijiji cha Tuikut kilichopo Sasur mkoani Bungoma nchini Kenya wameshitushwa kufuatia tukio la mwanamke mwenye umiri wa miaka 61 aitwaye Emily Psongonyo mkazi wa kijiji hicho kupigwa na shoti ya umeme na kusababisha kifo chake.

Tukio hilo limetokea Jumanne Septemba 7, Emily alikumbwa na shoti ya umeme kwenye uzio wa jirani yake alipokuwa anenda kupeleka maziwa Kanisa la karibu na hapo , amesema Mwenyekiti wa Mtaa Jackson Komon.

“ Nimepigwa simu asubuhi sa moja na moja mwanakijiji nilipofika eneo la tukio nimemkuta Emily akiwa amelala chini pamoja na Mbwa wawili wakiwa wamekufa kwa umeme” amesema Komon

Uwongozi wa shirika la umeme umefika eneo hilo na kugundua kuwa nyumba hiyo haitumi umeme wa halali , kijana Cleophas Nyoga alifahamika kuwa yeye ndo ameunga umeme huo alifanikiwa kutoroka baada kugundua amesababisha kifo cha Emily.

Pia wamesema,“ Tumeanzisha mpango wa kufatilia wanaounga umeme wa wizi na yotote atakayepatikana atachukuliwa hatua za kisheria ”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live