Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke atekwa zaidi ya mwaka Nigeria

Breaking Up On Facebook Mariaespievidal Mahusiano Facebook

Wed, 15 Jul 2020 Chanzo: Aljazeera

Mwanamke wa Marekani aliyehadaiwa na kupelekwa Nigeria kwa ahadi ya kuolewa na mwamume aliyekutana nae katika mtandao wa kijamii wa by Facebook ameokolewa baada ya kuzuiliwa mateka kwa zaidi ya mwaka mmoja, polisi wamesema.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46-alikuwa amefungiwa katika chumba cha hoteli kinyume na matakwa yake mjini Lagos.

Mshukiwa Chukwuebuka Obiaku, mwenye umri wa miaka 34, "alichukuwa umiliki wa kadi za benki za mwanamke huyo pamoja na fedha zake za kustaafu, kwa mujibu wa polisi.

Kwa zaidi ya kipindi cha 15 alilazimishwa kutoa jumla ya dola 48,000 sawa na (£38,000).

Mwanamke huyo alikuwa mtumishi wa umma aliyestaafu huko Washington DC

Polisi wanasema wanasema bwana Obiaku "alimtumia mwanamke huyo kufanya ulaghai kwa watu wanaouhusiana naye na raia wengine wa kigeni na makampuni.

Tunafahamu nini zaidi?

Mwanamke huyo aliwasili kutoka Marekani mwezi Februari 2019, kwa mujibu wa polisi wa Nigeria.

Mwezi Mei 2019 aliolewa na bwana Obiaku.

Kwa ujumla, mwanamke huyo alikuwa ameshikiliwa kinyume na matakwa yake kwa miezi 16 katika chumba cha hoteli.

Polisi wanasema walipata dondoo ya mwanamke huyo kutoka kwa raia mwema mmoja na hivyo kutumia taarifa hizo ili kumuokoa.

Bwana Obiaku amefungwa na polisi wamesema mtuhumiwa huyo anashtakiwa kwa makosa ya mtandao. Uhalifu mtandaoni ni ni mbaya kiasi gani?

Wahalifu hao waofahamika kwa jina maarufu kama "Yahoo boys", nchini Nigeria online fraudstewamekuwa wakiwatapeli watu mamilioni ya mtandaoni.

Mwezi uliopita, polisi wanasema wali walimuokoa mwanamke raia wa Ufilipino aliyezuru Nigeria kutafuta mpenzi baada ya kukutana na mwanamume Facebook.

Alizuiliwa kwa miezi sita bila hiari yake.

Kisa cha hivi karibuni kinahusisha matapeli wawili wa Nigeria waliokamatwa kwa madai ya wizi wamepelekwa Marekani na sasa wanasubiri kufunguliwa mashitaka.

Polisi wa Nigeria pia wametangaza kuwakamata wahalifu wengine watatu wanaohusishwa na wizi wa mtandaoni nchini Italia na Uturuki wanaoshukiwa kusambaza kwa njia isio halali barakoa za kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Polisi wanadai kuwa walipata zaidi ya dola 400,000 kutoka kwa wahalifu hao. Presentational grey line

Mtu hukuandikia baruapepe, akikuambia kuwa anataka umsaidie kutuma pesa

•Atakwambia kuwa matatizo ya kisiasa au matatizo ya majanga mengine vinamzuwia kutuma pesa

•Atakuomba umpe akaunti yako ili atume pesa

•Hii humsaidia kuifikia akaunti yako na kuweza kuondoa pesa

•Jihadhari sana na yale unayoyaandika katika mitandao ya kijamii kwani taarifa hizo huwasaidia kukufahamu vyema na kukukuleng

Chanzo: Aljazeera