Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke anayedai kufanya ngono na pepo

VENNIE Mwanamke anayedai kufanya ngono na pepo

Thu, 25 Jun 2020 Chanzo: BBC

Vennie Katoti anaposimulia maisha yake ya siku za nyuma, unaweza kudhani unatazama filamu ya kuogofya au kusikiliza hadithi za paukwa pakawa.

Lakini sivyo, ila anasema ni matukio halisi yaliyotokea katika maisha yake.

Vennie, binti mzaliwa wa Kenya ambaye kwa sasa ana miaka 31, anasema maisha yake ya utotoni yalikuwa ya kawaida hadi pale alipokutana na mpenzi wake wa kwanza. Je hali hii ilianza vipi?

Baada ya kumaliza masomo ya kidato cha nne, akiwa na miaka 18, alikutana na mwanaume ambaye walianza kupendana naye.

Usiku wa kwanza alioridhia kufanya mapenzi naye, hapohapo ndipo aliposhika mimba ya mtoto wake wa kwanza.

Vennie anasema kuwa mwanaume mwenyewe alikuwa na ari na hamu ya kumuoa kwani tayari alikuwa amempeleka nyumbani kwao akawaone wazazi.

Kwa wakati huo alipokuwa na mimba Vennie anakumbuka kuwa usiku mmoja aliingia kwenye ndoto ya kuwa amefanya mapenzi kwenye ndoto na mtu ambaye hakumuona.

Alipoamka asubuhi alihisi kuwa alikuwa na mwanaume lakini akimtafuta chumbani hamuoni. Ajabu iliyoje, alikuwa mwanaume wa ndoto.

"Wajua nilikuwa nimefanya mapenzi kwa mara ya kwanza na baba ya mtoto wangu kwa hivyo nilielewa jinsi hali hio hufanyika," anasema.

"Kwa hivyo nilipoamka asubuhi wakati pepo hilo liliponivamia na kushiriki mapenzi nami nilifahamu bayana ila sikujua la kufanya wala sikumwambia mtu yeyote." Mpenzi kutoroka

Wakati huo uhusiano wake na mwanamume aliyekuwa amempa mimba ulianza kudorora pindi tu alipoanza kufanya mapenzi na lile pepo.

Baada ya miezi miwili akiwa bado na ujauzito, uhusiano wake na mpenzi wake ulikuwa umeharibika kiasi cha kutoweza kunusurika.

Mpenziwe alitoroka asionekane tena.

Baada ya miezi 9 Vennie alijifungua mtoto mvulana ambaye kwa sasa ana miaka 9.

'Nilizaliwa na jinsia mbili'

Vennie anasema kuwa ile hali ya kufanya mapenzi na pepo iliendelea kwa muda wote aliokuwa na ujauzito na kuzidi kwa kasi baada ya kujifungua.

Anakumbuka kuwa ile hali ya kufanya mapenzi na pepo ilikuwa inafanyika kwenye ndoto na wala sio kwa hali halisia ya binadamu.

Kwa mfano wakati yuko kwenye shughuli zake za kawaida za mchana, hangeingiliwa na hali hii lakini pindi alipokuwa amelala basi ile hali ilikuwa inajirudia.

Vennie anasema kuwa wakati mwingine pepo yule alikuwa anashiriki mapenzi naye akiwa amejibadilisha na kuwa mnyama

"Nakumbuka kuwa kwa miezi sita hivi baada ya kujifungua niligundua uwepo wa nyoka mmoja katika ua la nyumba yetu. Nilikuwa wakati wote natamani kumuona, kwa hivyo nikawa na desturi ya kutoka nje na kusimama uani nikimsubiri," Vennie anasema

Wakati wa usiku nao desturi ikawa ni ileile ya pepo kufanya mapenzi naye kila wakati.

Vennie anasema kuwa ilikuwa vigumu sana kwake kufungukia watu kuhusu yaliyokuwa yanamkuta.

Kwanza kwa kuwa alipoanza kuwafungukia jamaa zake wa karibu na hata baadhi ya wachungaji, hawakumuamini, au walionekana kutaka tu kusikiliza masaibu yake bila kumpa suluhu yoyote.

Vennie anasema alijaribu suluhu za kiimani ili kukomesha hali hii katika maisha yake lakini ikawa ni vigumu mno.

Kwa mfano anasema kuwa ametembea makanisa na madhehebu mengi akitafuta suluhu na hata kujikuta katika vyumba vya ushirikina ila hakuna aliyetoa suluhu ya jinsi ya kuepukana na pepo huyo aliyekuwa amejitwika jukumu la kuwa "mume wake kiroho

"

Vennie anasema kuwa wengi wa watu ambao amewasimulia matukio haya ya maisha yake ya undani hawaamini ila ni hali halisi ambayo ameipitia. Uraibu wa kujichua

Vennie anasema kuwa kutokana na hali ya kuwa na urafiki wa ndani na pepo, haikuwa rahisi kwake kutangamana na wanaume.

Kila mara ambapo alipokumbana na mtu ambaye alikuwa anaonyesha dalili za kumpenda au kumchumbia, uhusiano huo ulikuwa unaharibika na asijue sababu kuu ya hayo kufanyika .

Katika pilikapilika hizo za mahusiano hayo ambayo sio kawaida na maumbile ya binadamu Vennie anasema kuwa alianza tabia mpya ya kujichua.

Mshiko huu wa kujichua ulikuwa mbaya sana kwani anasema kuwa ulikuwa unamsukuma kila wakati

"Nakumbuka siku zilizopita nilikuwa tu naharakisha kufika nyumbani wakati fulani kutokana na mshawasha wa kumaliza kiu kwa kujichua," Vennie anasema

Katika hali hii ya kujichua Vennie anakiri kuwa alianza kuwa na tabia ambayo sio ya kawaida, ambayo ilimpelekea yeye kuwatesa wapenzi wake.

Aliwahadaa wengi kimapenzi hadi pale baadhi yao walipoanza kuingiliwa na uraibu huo huo wa kujichua

'Mume wangu alizoea kunilawiti na kunibaka' 'Nilibakwa na wanaume watatu siku ya harusi yangu'

Kukombolewa

Vennie anakiri kuwa tabia hii ya kushiriki mapenzi na pepo na kujichua pia ilimfanya mnyonge na pia akawa amejitenga sana na watu.

Alijihisi mchafu na asiyekubalika katika jamii.

Vennie anasema kuwa alianza kufanya maombi ya kila siku -huku akimshirikisha dada yake pamoja na wanawake wengine kama njia ya kujiokoa kutoka kile anachokitaja kama mtego wa shetani.

Kwa siku hizo anasema kuwa alikiri kwa maneno kuziasi njia za kukubali kufanya mapenzi na pepo pamoja na hali hii ya kujichua .

Na kwa kweli kwa sasa anasema kuwa kwa muda sasa hali hii haijajirudia tena. Hali kadhalika ameacha uraibu aliokuwa nao wa kujichua .

Vennie anahusika sana kwa sasa na kuzungumzia wazi tabia hii ambayo anasema kuwa imo kwenye jamii lakini haizungumziwi wazi wazi kwani watu wanapuuza tu kama ndoto.

Inawezekana kufanya mapenzi na pepo?

Hili ni jambo embalo limezua mijadala na dini mbalimbali hata katika fani za wasomi , Wanasaikolojia na viongozi wa kidini wanatofautiana kuhusu hili.

Saikolojia inahoji kuwa tabia hii hutokana na mawazo ya mtu yalivyo, ikiwa mtu atawazia hali ya kufanya mapenzi na ngono kila wakati basi huenda mawazo aliyokuwa nayo yakamuingilia kwenye ndoto zake.

Wanasema tabia kama hii ya Vennie Kakoti ambaye amekiri kuwa katika jamii yao walitafuta usaidizi wa ushirikina na uchawi kila wakati, sio ajabu kuwa maisha ya vennie yalikuwa na mlango wa pepo kuingia ndani yake na kuanza kumdhulumu bila idhini yake .

Aidha watu wanaokuwa na tabia za uraibu kama wa kujichua , ngono na unywaji wa pombe au madawa ya kulevya kupindukia , huwa wameanza tu kama mzaha lakini tabia hii inakuwa ya kila siku . Hatimaye wanajipata hawawezi kutoka katika mtego wa tabia hizi .

Je nini husababisha matukio kama haya ?

Kulingana Mchungaji T Mwangi ambae anahusika sana na kutoa motisha , ana uzoefu wa kuzungumzia hatua za kubadilisha tabia na ujenzi wa maadili na pia mzungumzaji dhidi ya tabia zinazohusu uraibu wa ngono na kadhalika anasema kuwa jamii ambazo zinaenzi tabia ya ushirikina, uchawi na kadhalika hufungua milango kwa nguvu za giza au kishetani kuingilia maisha yao na kutawala kila sekta ya maisha. Hii ni pale mtu anapotafuta pengine kujaaliwa fedha Zaidi au anapotafuta njia za mkato za kutafuta penzi .

Bwana T anasema tabia kama hii ya Vennie Kakoti ambaye amekiri kuwa jamii yao walitafuta usaidizi wa ushirikina na uchawi kila wakati, sio ajabu kuwa maisha ya vennie yalikuwa na mlango wa pepo kuingia ndani yake na kuanza kumdhulumu bila idhini yake .

Aidha Bwana T anasema kuwa watu wanaokuwa na tabia za uraibu kama wa kujichua , ngono na unywaji wa pombe au madawa ya kulevya kupindukia , huwa wameanza tu kama mzaha lakini tabia hii inakuwa ya kila siku . Hatimaye wanajipata hawawezi kutoka katika mtego wa tabia hizi . Mchungaji T anahoji kuwa maombi yana nguvu juu ya tabia na mishiko ya aina hii , ila bidii kutoka kwa mtu aliyetekwa ya kutaka kuachana na tabia hizo lazima iwepo .

Chanzo: BBC