Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke aliyeteuliwa kuwa Waziri Mkuu kwa mara ya kwanza Tunisia

Najla Bouden Romdhan Rais wa Tunisia amteua mwanamke kama waziri mkuu kwanza kwa ulimwengu wa Kiarabu

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tunisia Kais Saied amemteua Najla Bouden Romdhan kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Tunisia na nchi za Kiarabu, miezi miwili baada ya kuifuta serikali iliyotangulia na kutwaa mamlaka nchini humo.

"Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tunisia kwa mwanamke kuongoza serikali," Saied amesema alipokutana na Romdhan Jumatano, kulingana na video kutoka ofisi ya Rais. "Ni heshima kwa Tunisia na wanawake wa Tunisia."

Romdhan mwenye umri wa miaka 63 amefanya kazi katika wizara ya elimu ya juu kwenye miaka ya 2011, kwa mujibu wa taarifa za kituo cha radio cha Mosaique FM cha Tunisia.

Romdhan anaingia madarakani wakati nchi ikiwa kwenye mgogoro, pamoja na mafanikio ya kidemokrasia yaliyopatikana wakati wa mapinduzi ya 2011 huku nchi ikiwa kwenye mashaka na tishio kubwa la fedha la serikali, ingawa kuna maswali juu ya nguvu gani atakuwa nayo.

Mnamo Julai, Saied aliiondoa serikali na kuzuia shughuli za bunge lililoongozwa na chama cha Kiislam cha Ennahda, hatua ambayo maadui wake waliita mapinduzi. Wiki iliyopita alipuuza misingi minhi ya katiba, akisema anaweza kutawala kwa amri na kudhibiti serikali mwenyewe wakati wa kipindi cha dharura ambacho hakina mwisho.

Tunisia inakabiliwa na mgogoro unaokuja kwa kasi katika fedha za umma baada ya miaka kadhaa ya kudorora kwa uchumi kuchochewa na janga la coronavirus na mzozo wa kisiasa.

Serikali mpya italazimika kufanya kazi kwa haraka sana kutafuta msaada wa kifedha kwa bajeti na ulipaji wa deni baada ya kuchukua madaraka kwa nguvu mnamo Julai hivyo wanapaswa kuanza mazungumzo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live