Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke aliyerudi shule na miaka 40 ahitimu!

Mwanamke 40 Ahitimu (600 X 312) Mwanamke aliyerudi shule na miaka 40 ahitimu!

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akiwa na miaka 40 mnamo mwaka 2019, Gladys Gakii maarufu kama Conje alikata shauri na kurudi shuleni (sekondari) kwa ajili ya kuisaka elimu huko nchini Kenya, ambapo sasa amehitimu stashahada.

Tovuti ya Tuko imeripoti kuwa safari ya Conje katika elimu haikuwa rahisi kwani alilazimika kurudi shule baada ya biashara na mali zake kupotea, hata hivyo alivyoamua kurudi shule bado alipitia changamoto za ada tangu akiwa sekondari hadi Chuo Kikuu.

"Nimehitimu Diploma ya Makosa ya Jinai na Mafunzo ya Usalama. Baada ya kuhangaika na ada ya shule, Makamu Mkuu wa chuo aliona nia na kiu yangu ya elimu na akanipa ufadhili wa masomo Desemba mwaka jana," amesema.

"Mnamo Januari 2023, kwa neema ya Mungu, nitanza shahada yangu ya kwanza, namshukuru Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tharaka profesa Peter Kinyua Muriungi kutokana na mchango wake katika safari yangu," ameongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live