Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke akamatwa akiingiza bangi jela

Mka Bangi Mwanamke akamatwa akiingiza bangi jela

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 30, alikamatwa Jumapili, Novemba 27, baada ya kupatikana akijaribu kuingiza bangi ndani ya seli ya polisi.

Mwanamke huyo anasemekana kufika katika Kituo cha Polisi cha Gilgil mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi ili kumtembelea mume wake, ambaye alikuwa kwenye seli.

Hata hivyo, njama yake ilitibuliwa wakati mmoja wa maafisa wa polisi waliokuwa wakisimamia seli hiyo alipogundua vifurushi vya bangi vilivyofichwa ndani ya nguo zake za ndani na kwenye mkate.

"Mwanamke mpole ambaye alikuwa na sura ya mke mwema na matendo yake yalionekana kuwa yenye wema, alikuwa amebeba mkate na chupa iliyojaa chai moto, ili kukabidhiwa kwa mumewe kwa kifungua kinywa," ripoti ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilisoma kwa sehemu.

Japo alionekana mtu asiye na hatia, afisa mmoja wa kike alitilia shaka mlo uliokuwa umepakiwa na akaamua kuchunguza zaidi yaliyokuwa ndani.

"Afisa aliyekuwa kwenye zamu hakushawishiwa na tabia ya mwanamke huyo. Alifunua mkate huo na kupata mkate wa kisasa lakini mwishowe, aligundua vifurushi vitano vya bangi, sigara tano na kiberiti," wapelelezi walisema.

Alielekezwa kuingia kwenye chumba kilichokusudiwa kwa ajili ya kesi zinazohusiana na jinsia ili kufanyiwa uchunguzi wa kina katika mwili wake kutambua iwapo aliweza kuficha dawa zingine ndani ya nguo zake.

Akithibitisha shaka yake, afisa huyo alipata vifurushi 80 vya bangi vikiwa vimefichwa kwenye nguo zake za ndani.

Isitoshe, mwanamke huyo pia anadaiwa kujaribu kuhonga afisa huyo ili aachiliwe, na kujiongezea makosa zaidi.

"Juhudi za mshukiwa kuwahonga maafisa hao KSh2,000 (Tsh 38,000) ili kupata uhuru wake hazikukatiliwa tu bali pia alijiongea mashtaka zaidi," iliongeza ripoti hiyo.

Sawia na mumewe ambaye pia anazuiliwa kwa kosa la kumiliki bangi na kujaribu kuipenyeza ndani ya seli, mwanamke huyo pia alizuiliwa kwenye seli.

Kwa sasa mshukiwa huyo anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Gilgil akisubiri kufikishwa mahakamani leo Jumatatu, Novemba 28 asubuhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live