Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke abakwa na wanaume watatu waliojifanya maofisa wa polisi

Crime Scene 45.jpeg Mwanamke abakwa na wanaume watatu waliojifanya maofisa wa polisi

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 27 alishambuliwa na kubakwa na wanaume watatu waliojifanya maafisa wa polisi.

Kisa hicho kilitokea kwenye njia ya giza kutoka eneo la Kiwanja kuelekea Kahawa West mnamo Jumatatu, Desemba 12, mwendo wa usiku.

Mwanamke huyo aliwaambia polisi kuwa alikuwa pamoja na mpenzi wake na walikuwa wakielekea nyumbani walipokabiliwa na wanaume watatu.

Wawili hao walikuwa wamenunua chakula madukani na walikuwa wakielekea nyumbani walipokabiliwa na wanaume waliodai kuwa walikuwa maafisa wa polisi.

Waathiriwa walisema watatu hao waliwaamuru wasijaribu kutoroka.

Waliwaamuru wawili hao kulala chini katika uwanja wazi kabla ya kuanza kumbaka mwanamke huyo huku mpenzi wake akitazama bila la kufanya.

Watatu hao walikuwa wamejihami kwa visu.

Genge hilo baadaye lilitoroka baada ya kutekeleza uhalifu wao ya kuwaacha wawili hao katika eneo la tukio.

Mwanamke huyo alipelekwa katika hospitali ya Juja ambako alihudumiwa na kuruhusiwa.

Timu ya wapelelezi imepewa jukumu la kuwinda genge hilo.

Mkuu wa polisi wa Kiambu Perminus Kioi alisema bado hawajajua nia ya shambulio hilo.

Alisema maafisa hao wanachunguza nia hiyo kwa nia ya kuwapata wabakaji.

Kesi za ubakaji zimekuwa zikiongezeka nchini.

Kwa mfano, kesi za ubakaji ziliongezeka hadi 973 mwaka 2020 ikilinganishwa na 950 zilizoripotiwa mwaka 2019, 921 mwaka 2018, 784 mwaka 2017 na 923 mwaka 2016.

Kesi za unajisi ziliongezeka hadi 6,801 mwaka 2020 kutoka 5,397 mwaka 2019, 4,767 mwaka 2018, 3,487 mwaka 2017 na 4,512 mwaka 2016.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live