Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke Zimbabwe apigania mashine itengenezwe ili asikate matiti

BreastCancerAI.png Mwanamke Zimbabwe apigania mashine itengenezwe ili asikate matiti

Mon, 13 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke wa miaka, 44, nchini Zimbabwe, Tendayi Gwata, inakabiliwa na tishio la kukatwa matiti baada ya matibabu yake ya saratani kukatizwa ghafla.

Hiyo ni baada ya mashine moja pekee ya tiba ya saratani ya njia ya miale ya 'radiotherapy' katika mji mkuu wa Harare, kuharibika.

Bi. Gwata ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mauzo tayari amepoteza nywele zake kichwani wakati akifanyiwa tiba ya chemotherapy.

Sasa ameambiwa huenda akakatwa matiti kwa sababu mashine imeharibika.

Sekta ya afya nchini Zimbabwe imeathiriwa pakubwa na kuzorota kwa uchumi ambako kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumko wa bei kwa hadi aslimia 785 na uhaba wa fedha.

Mdororo wa kiuchumi umekuwa mbaya zaidi kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Bi. Gwata amemsimulia hali yake mwandishi wa BBC Clare Spencer. Short presentational grey line

Mwezi Julai 2019 nilihisi maumivu kwenye titi langu nikaamua kwenda kumuona daktari mjini Harare ambapo nilifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Matokeo ya uchunguzi huo yalibaini naugua saratani ya matiti ambayo imesambaa hadi chini ya kwapa langu.

Nilisafiri nchini Afrika Kusini kwa matibabu yaliyojumuisha kuondolewa kwa uvimbe kwenye titi langu.

Niliporudi nyumbani Harare, nikaanza tiba ya radiotherapy ili kuzuia uvumbi usirejee tena.

Wakati tulipoenda kuulizia tiba hiyo, tulifahamishwa ni mashine moja tu ndio inafanya kazi kote mjini Harare na inapatikana katika hospitali ya kibinafsi ya Oncocare.

Nilikuwa nimepiga hatua kubwa katika matibabu yangu - tayari nilikuwa nimefanyiwa tiba hiyo mara 21 kati ya 30 nilizohitaji kufanyiwa. Kupigiwa simu.

Nilikuwa njiani kuelekea kwa tiba yangu ya 22 wakati nilipopigiwa simu kufahamishwa nikatize safari kwa sababu mashine imeharibika.

Ilikuwa Aprili 21. Wiki ya kwanza ikapita. Mwezi ukapita. Na mpaka sasa sina hakika ni lini mashine hiyo itarekebishwa.

Daktari wangu sasa amenishauri nianze kutafakari uwezekano wa kufanyiwa upasuaji wa kukatwa ziwa langu.

Nilijizuia sana kutolia.

Nimejizatiti sana kuishi na hali yangu ya afya na kuchukulia ugonjwa huu kama changamoto za kawaida za maisha na kuwa na matumaini nikisema: "Nitanusurika kifo kutokana na ugonjwa huu," inasikitisha juhudi zote hizi zinaishia mimi kufikia kiwango cha kukatwa titi kwa sababu hakuna mtu wa kutengezeza mashine ambayo ingeniepusha na oparesheni hiyo.

Kusema kweli nilijihisi kuangua kilio lakini ghadhabu yangu ilinielekeza katika mtandao wa kijamii wa Twitter ambako niliangazia hali inayonikabili na changamoto ninayopitia.

Pia nilianza kujifunza mambo mengi kuhusu aina ya tiba ya saratani inayofahamika kama radiotherapy.

Lakini kila nilivyoendelea kusoma nilipatana na maelezo yalioangazia hatari ya kukosa aina hiyo ya tiba baada ya siku mbili.

Katika utafiti niliokuwa nafanya mitandaoni, sikupata matokeo ya uchunguzi wowote unaoangazia hatari ya kukosa radiotherapy kwa miezi miwili ama mitatu.

Hata ni vigumu kupata matokeo ya uchunguzi kama huo kwa sabau mashine ya tiba muhimu kama hii haiwezi kuachwa ikiwa na hitilafu kwa muda mrefu hivyo.

Nilipomsimulia mwandishi wa BBC masaibu yangu katika mahojiano ya kipekee nilipokea simu kutoka kwa watu kadhaa wakinuuliza: "Tunaweza kukusaidiaje? Tukusaidi vipi?"

Niliwaelezea kuwa nimeshindwa kuwasiliana na mtu ambaye anaweza kunipatia majibu na ambaye pia anaweza kunielezea hatua itakayofuata.

Kwa hivyo, mmoja wa marafiki zangu tuliyesoma pamoja shule ya upili amenipa nambari ya simu ya mkuu wa bodi ya matibabu ambaye hatimaye aliniunganisha na Ernest Manyawo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Hospitali kuu ya umma Harare, Parirenyatwa. Sio tu Mimi

Hapo ndipo niligundua ukubwa wa tatizo hili. Aliniambia kwamba kuna watu 500 ambao kwa sasa wapo nyumbani kwa sababu mashine za tiba ya saratani zimeharibika.

Sio mimi pekee yangu. Na Sio watu wachache wanaokabiliwa na changamoto kama yangu bali ni mamia ya watu, kwa kweli hili ni jambo la kuhuzunisha sana. Ghadhabu yangu inatokea hapo.

Kutokana na hali niliopitia mimi binafsi nafahamu fika changamoto inayotokana na safari ya kutafuta tiba ya saratani kutafuta fedha ya kuanzia matibabu, upasuaji hadi kuchangisha fedha za kuendeleza matibabu.

Huu ni mzigo mkubwa kwa familia na inavuja moyo kwamba baada ya mahangaiko yote hayo mgonjwa anakosa matibabu kwasababu mashine imeharibika.

Mwanzoni nilipokuwa natafuta sehemu ya kuendeleza tiba yangu baada ya kurejea nchini kutoka Afrika Kusini nilielekezwa, Parirenyatwa na wala sikupewa hospital nyingine mbadala.

Baadaye nilifahamishwa kuwa wana mashine tatu lakini zote zimeharibika tangu mwaka mwaka 2019 hazijafanya kazi. line Pia unaweza kusoma:

Mpasuaji wa saratani ya matiti aliyepata saratani ya matiti Wanawake katika hatari ya kuugua saratani wahitaji ukaguzi wa mapema

line

Bw. Manyawo aliniambia kuwa wamepokea vifaa vya kutengeneza mashine hizo mwezi Februari.

Mashine hizi zinagharimu kati ya dola milioni moja sawa na (£795,000). Masharti ya kutoka kwa kampuni iliyonunuliwa ni kwamba watakaotengeneza ikiharibika ni wahandisi wao pekee.

Lakini wahandisi wako Afrika Kusini. Sijalala vizuri

Bw. Manyawo hakunieleza kwa nini imewachukua miezi sita kupata vifaa vya kutengeneza mashine na hiyo ndio sababu wahandisi hawakufika kuzitengeneza punde tu baada ya kuwasili.

Kisha Machi 23, kabla ya wahandisi kuwasili, Zimbabwe ikafunga mipaka yake katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Sasa nimefahamishwa kuwa wahandisi hao wamekatiwa tiketi lakini ndege inasubiri idhini ya Wizara ya Afya.

Kwa sasa tumesalia na kizungumkuti hicho. Nasononeka moyoni mwangu. Sipati usingizi. Naamka katikati ya usingizi usiku.

Lakini najaribu kupata lepe la usingizi kwa sababu ugonjwa wa saratani umenipa funzo moja maishani - kwamba nisiwe na hofu katika kila hatua ya safari ya tiba kwani ni safari ndefu.

Ama utatumia maisha yako yote kuwa na wasiwasi na hivyo sio vizuri kwa afya yako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live