Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke Mkenya akamatwa akiwa ameficha dhahabu kwenye nguo ya ndani

Pingu Selo 660x400 Mwanamke Mkenya akamatwa akiwa ameficha dhahabu kwenye nguo ya ndani

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mwanamke Mkenya mwenye umri wa miaka 40 alikamatwa Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Mumbai, India kwa madai ya kusafirisha kilo 3.4 za dhahabu yenye thamani ya Sh29 milioni.

Kitengo cha Ujasusi cha hewa (AIU) kilisema kuwa mwanamke huyo alikuwa ameficha dhahabu hiyo kwenye nguo yake ya ndani na alikuwa akitoka nje ya uwanja wa ndege ndipo aliponaswa.

Maafisa wa forodha waligundua vipande 17 vya dhahabu zilizoyeyushwa zenye karati 22 zikiwa zimefichwa kwenye nguo yake ya ndani, pamoja na pande mbalimbali vya karati 21 vilivyofichwa mwilini mwake, wakati wa ukaguzi wa mizigo yake.

Maafisa walisema alikuwa ameondoka Nairobi Septemba 30, kuelekea Mumbai. Anaaminika kuwa sehemu ya harambee kubwa ya magendo ya dhahabu iliyoko Mumbai, mahali ambapo maafisa wanaiita kitovu cha wasafirishaji dhahabu.

Mnamo Aprili mwaka huu, wanawake tisa wa Kenya walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Mumbai kwa kujaribu kusafirisha dhahabu yenye thamani ya Sh156.4 milioni. Kwa mujibu wa habari, takriban kilo 640 za dhahabu zenye thamani ya Sh6 bilioni (zaidi ya milioni 360) zimenaswa katika uwanja wa ndege.

Makundi mbalimbali yanasemekana kuwatumia wanawake wa kigeni kuingiza dhahabu nchini humo. Kulingana na sheria za India, ni kosa la jinai kubeba dhahabu iliyofichwa.

Chanzo: Radio Jambo