Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke Mganda anayejihusisha na mapenzi jinsia moja apewa hadhi ya ukimbizi

Mwanamke Mganda Anayejihusisha Na Mapenzi Jinsia Moja Apewa Hadhi Ya Ukimbizi Mwanamke Mganda anayejihusisha na mapenzi jinsia moja apewa hadhi ya ukimbizi

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mwanamke mmoja kutoka Uganda ambaye alidai aliteswa kwa kuwa mpenzi wa jinsia moja amepata hifadhi ya kuwa mkimbizi nchini Japani baada ya mahakama kutupilia mbali agizo la serikali la kufukuzwa nchini mwake.

Alikuwa amewasili Japani mwaka 2020 akisema polisi wa Uganda walikuwa wamemshambulia kwa sababu ya jinsia yake.

Lakini ombi lake lilikataliwa na serikali ya Japan ambayo iliidhinisha maombi 200 ya hifadhi mwaka jana.

Tokyo - ambayo imekosolewa kwa kuchukua wakimbizi wachache sana kuliko mataifa mengine yaliyoendelea kiviwanda imekuwa ikijaribu kufanya mchakato wa kupata hifadhi kwa uwazi zaidi.

Kifo cha wanawake wa Sri Lanka katika kituo cha wahamiaji mnamo 2021 kilisababisha taifa hilo kukosolewa zaidi.

Chanzo: Bbc