Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke Anaswa Akiingia Leba Kuiba Mtoto

Mtoto12 Mtoto

Sat, 25 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWANAMKE mmoja aliyejifanya mjamzito na kujaribu kuingia kwenye wodi ya akina mama wajawazito wanaotakiwa kujifungua katika Hospitai ya Taifa ya Kenyatta (KNH), Elizabeth Musembi amekamatwa jana Ijumaa, Septemba 24, baada ya kushukiwa alikuwa anapanga kutekeleza wizi wa mtoto.

Akizungumza na vyombo vya habari, Musembi alieleza kwamba kwamba alikuwa na hamu kubwa ya kupata mtoto baada ya kujaribu kupata ujauzito kwa miaka mingi bila mafanikio.

"Kuna dada alikuwa ameniahidi kwamba atanibebea ujauzito lakini wakati siku za kujifunua zilipofika, alitoweka. Lengo langu kuingia KNH haikuwa kuiba mtoto lakini kuangalia iwapo nitampata mtoto ambaye ametorokwa na mamake," alijitetea.

OCPD wa Kilimani, Andrew Muturi amesema kwamba Musembi huenda angeiba mtoto iwapo maofisa hao wa usalama hawangekuwa macho.

"Tumemkamata na tunakwenda kumfanyia uchunguzi wa kimatibabu na baada ya hapo tutaamua atafunguliwa mashtaka ya aina gani," Muturi alisema. Kwa sasa Musembi anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimani akisubiri kufikishwa mahakamani Jumatatu wiki ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live