Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamfalme Phillip alazwa hospitali kwa uangalizi

1e8b49d9561698dde0b712613ede2c70 Mwanamfalme Phillip alazwa hospitali kwa uangalizi

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANAMFALME wa Uingereza, Phillip ambaye pia ni Mtawala wa Edinburgh amelazwa hospitalini tangu Jumanne wiki hii kwa uangalizi wa karibu baada ya kutojisikia vizuri.

Taarifa ya Makao Makuu ya Ufalme, Buckingham Palace, ilieleza kuwa Mwanamfalme Phillip mwenye miaka 99, alilazwa kwa tahadhari katika Hospitali ya King Edward VII, mjini London.

Inaelezwa kuwa hata hivyo anaendelea vizuri baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo na kufafanua kwamba, kinachomsumbua hakina uhusiano na homa kali ya mapafu (Covid-19) na madaktari wameshauri aendelee kuwepo hospitali kwa uangalizi zaidi.

Mwezi uliopita, Kasri ya Kifalme ilitangaza kuwa, Mwanamfalme Philip na Malkia mwenye miaka 94, walipewa chanjo ya Covid-19 kutoka kwa daktari wa Ufalme katika Kasri lao na Windsor Castle aliko Malkia mpaka sasa.

Desemba mwaka 2019, Mwanamfalme Philip alilazwa kwa siku nne katika hospitali hiyo ya King Edward VII kwa hatua ya tahadhari na matibabu.

Baadaye aliruhusiwa kuondoka hospitalini siku moja kabla ya Krismasi na kusafirishwa kwa gari hadi katika makazi ya Sandringham ambako alisherehekea sherehe hiyo na Malkia.

Msemaji namba 10 wa Ufalme alisema Waziri Mkuu, Boris Johnson alituma salamu za pole kwa Mwanamfalme na kumtakia afya njema wakati akiendelea na uangalizi hospitalini.

Matibabu ambayo ameyapata kutokana na hali tofauti za kiafya kwa miaka tofauti mpaka sasa ni pamoja na kuziba kwa mishipa ya uti wa mgongo mwaka 2011, maambukizi ya kibofu cha mkojo mwaka 2012, na upasuaji wa tumbo kwa ajili ya uchunguzi uliofanyika Juni 2013.

Chanzo: habarileo.co.tz