Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanajeshi wa Uganda auawa makabiliano ya kundi la ADF

Mwanajeshi Wa Uganda Auawa Makabiliano Ya Kundi La ADF Mwanajeshi wa Uganda auawa makabiliano ya kundi la ADF

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: Voa

Mwanajeshi wa Uganda ameuawa katika makabiliano na waasi wa kundi la Allied democratic forces ADF waliovuka mpaka kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kuingia katika wilaya ya Ntoroko, magharibi mwa Uganda.

Msemaji wa jeshi la Uganda Brig Felix Kulayigye amethibitisha kwamba mwanajeshi mmoja ameuawa pamoja na waasi 11.

Jeshi la Uganda limesema kwamba kundi la waasi karibu 30 lilivuka mto Semuliki na kuingia sehemu za wilaya za Kyanja na Ntoroko, kabla ya kukabiliwa na wanajeshi wa Uganda.

Waasi 8 wamekamatwa na bunduki 10 kupatikana.

Hii ni mara ya kwanza tangu miaka ya 1990 waasi wa ADF wamevuka mpaka na kuingia Uganda kutoka DRC.

Wanajeshi wa Uganda wanafanya oparesheni maalum ndani ya DRC dhidi ya waasi wa ADF, ambao kamanda wao mkuu Jamil Mukulu anazuiliwa Uganda baada ya kukamatwa nchini Tanzania mwaka 2015.

Kundi hilo sasa linaongozwa na Musa Baluku. Inaripotiwa kwamba kundi hilo limegawanyika katika makundi mawili. kundi moja linaunga mkono Jamil Mukulu aliye gerezani na linginge linaongozwa na Baluku.

Wakati huo huo, muungano wa jeshi la DRC na Uganda umetangaza kuokoa raia 74 kutoka mikononi mwa kundi la ADF baada ya kuua waasi 30.

ADF ni kundi la waasi lililoanzia Uganda likipambana na utawala wa rais Yoweri Museveni, kabla ya kukimbilia Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ambapo limejificha.

Limekuwa likitekeleza mashambulizi nchini Uganda na kukimbilia DRC.

Maafisa wa usalama wa Uganda wamehusisha kundi la ADF na mauaji ya maafisa wa ngazi ya juu serikalini, wakiwemo maafisa wa polisi na jeshi.

ADF limehusishwa na mauaji ya mamamia ya watu nchini DRC kila mwaka.

Chanzo: Voa