Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanajeshi wa Mali ashikiliwa kutokana na kitabu kinachodai kukiuka haki za kijeshi

Mwanajeshi Wa Mali Ashikiliwa Kutokana Na Kitabu Kinachodai Kukiuka Haki Za Kijeshi Mwanajeshi wa Mali ashikiliwa kutokana na kitabu kinachodai kukiuka haki za kijeshi

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Kanali mmoja katika jeshi la Mali ametiwa mbaroni kutokana na kitabu chake kilichotolewa hivi karibuni, ambacho kilikuwa na madai kuwa jeshi limefanya ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia.

Katika kitabu hicho chenye kurasa 400 chenye kichwa cha 'Mali: Changamoto ya Ugaidi katika Afrika', Kanali Alpha Yaya Sangaré, akinukuu mashirika ya haki za binadamu, aliandika: "Tangu 2016, FDS [Vikosi vya Ulinzi na Usalama] vimejihusisha na unyanyasaji dhidi ya watu wanaotuhumiwa kuwa sehemu. wa makundi ya kigaidi".

Aliongeza kuwa wanajeshi walifanya unyanyasaji huo "kwa ushirikiano wa uongozi wa kijeshi".

Bw.Sangare alikamatwa Jumamosi jioni, lakini kukamatwa kwake kulithibitishwa na familia yake siku ya Jumapili.

Wizara ya ulinzi ya Mali Ijumaa iliyopita ilishutumu madai hayo yaliyochapishwa katika kitabu hicho, na kuyataja kuwa ya "uongo".

Mashirika kadhaa ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameshutumu wanajeshi wa Mali kwa kuwadhulumu na kuwanyonga raia katika mapambano yao dhidi ya waasi wa Kiislamu.

Chanzo: Bbc