Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanajeshi wa Kenya auawa katika shambulio la waasi DR Congo

Mwanajeshi Wa Kenya Auawa Katika Shambulio La Waasi DR Congo Mwanajeshi wa Kenya auawa katika shambulio la waasi DR Congo

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mwanajeshi wa Kenya aliye katika kikosi cha jeshi la Afrika Mashariki mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameuawa kufuatia shambulio la kuvizia na waasi.

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Patrick Muyaya aliiambia BBC kwamba mwanajeshi huyo alifariki siku ya Jumanne wakati wa mapigano kati ya wanajeshi wa eneo hilo na waasi wa M23 katika eneo la Kibumba.

Ni kifo cha kwanza kuripotiwa miongoni mwa wanajeshi wa Kenya tangu wajiunge na kikosi hicho mwaka jana.

Taarifa kutoka kwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ililaani mauaji hayo, na kuwalaumu M23.

Ilisema waasi hao walifyatua kombora katika ngome za Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF).

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilisema shambulio hilo lililenga "kuzua kutoelewana" kati yake na EACRF.

Waasi wa M23 hawajatoa tamko lolote kuhusiana na shutuma hizo.

Mapigano yameanza tena hivi majuzi kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wanaojulikana kwa jina la Wazalendo katika maeneo ya jimbo la Kivu Kaskazini.

Kikosi cha kikanda kimekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka DR Congo kwa kushindwa kukomesha ghasia.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema haitaidhinisha upya mamlaka ya EACRF, ambayo itakamilika mwezi Desemba.

Kenya imechangia zaidi ya wanajeshi 1,000 katika ujumbe huo ambao pia unajumuisha wanajeshi kutoka Uganda, Sudan Kusini na Burundi.

Chanzo: Bbc