Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanajeshi atupwa jela miaka 10 kwa kumtishia maisha trafiki

 Emmanuel Chakwanda D21b Emmanuel Chakwanda.

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanajeshi Emmanuel Chakwanda amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela kwa kutishia kumshambulia Afisa wa Polisi anayesimamia usalama barabarani (trafiki) huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Uamuzi wa Mahakama ya Kijeshi ya Ngaliema mjini Kinshasa ulitolewa baada ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonyesha askari huyo akimnyooshea afisa wa Polisi silaha yake na kufyatua risasi hewani.

Watu wamelaani mwenendo wa askari huyo bila kusahau mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live