Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanajeshi asakwa baada ya kuwapiga risasi na kuwaua watu 13

Mwanajeshi Asakwa Baada Ya Kuwapiga Risasi Na Kuwaua Watu 13 Mwanajeshi asakwa baada ya kuwapiga risasi na kuwaua watu 13

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Mwanajeshi mmoja anasakwa katika jimbo la Ituri baada ya kurejea nyumbani kutoka kazini siku ya Jumamosi na kuwapiga risasi watu 13, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, kulingana na mamlaka.

Luteni Jules Ngongo, msemaji wa utawala wa kijeshi katika mkoa wa Ituri, aliyaambia magazeti ya nchini humo kuwa "popote [askari] atakapokwenda, tutamkamata".

Kulingana na magazeti katika eneo hilo kati ya watu 13 waliofariki, tisa (9) ni watoto, huku taasisi ya inayofuatilia masuala ya kiusalama katika jimbo la Kivu Baromètre Sécuritaire du Kivu ikisema kuwa wawili ni wanawake.

Askari huyo wa jeshi la serikali anatuhumiwa kuwaua watu hao Jumamosi usiku katika eneo la Tchomia karibu na Ziwa Albert jimbo la Ituri.

Ni nini kilimchochea?

Majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini yamekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu 2021

Gazeti la Bunia-Actualité linaripoti kwamba askari huyo aliondoka eneo alilokuwa akifanya kazi na kwenda nyumbani baada ya kupata habari kwamba mwanae amefariki.

Inasemekana mwanae alifariki Alhamisi tarehe 20 na akazikwa Ijumaa jioni, bila baba yake kufika.

Mwanawe alidaiwa kufariki dunia kwa kifo cha kawaida baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Tchomia ambako alifariki dunia.

Baba aliporudi nyumbani na kumkuta mtoto wake amezikwa, alikasirika na kupiga risasi kati ya majirani waliofika kuifariji familia.

Radio Okapi inaripoti kuwa miongoni mwa wengine waliopigwa risasi na mwanajeshi huyo ni watoto wake wawili.

Luteni Ngongo anasema hilo ni suala la ‘kinidhamu’. Anasema askari huyu akikamatwa atashitakiwa mahakamani.

Chanzo: Bbc