Mwanaharakati aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi, Spika wa Bunge la kwanza la Afrika Kusini lililochaguliwa kidemokrasia na mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo, Frene Ginwala amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.
Taarifa kutokana Ofisini ya Rais wa Afrika Kusini iliyotolewa kwa Taifa, imesema mtaalamu huyo wa katiba alifariki nyumbani kwake usiku wa Januari 12, 2023 baada ya kuugua kiharusi wiki mbili zilizopita.
Ginwala, alizaliwa jijini Johannesburg katika jamii ya Kihindi ya Afrika Kusini na kusomea sheria nchini Uingereza ambapo baadaye aliteuliwa kuwa spika wa bunge mwaka wa 1994, wakati Nelson Mandela alipo chaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo.
Kuchaguliwa kwa Mandela kuwa Rais wa Taifa hilo, kulihitimisha rasmi utawala wa watu weupe ambao walisifika kwa ubaguzi wa range na Spika huyo alihudumu nafasi hake hadi mwaka 2004 alipostaafu rasmi.