Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaharakati mwanamke afungwa miaka 15 jela Rwanda

Idamange Yvonna Idamange Yvonna

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: BBC Swahili

Mahakama ya mjini Nyanza kusini mwa Rwanda imemhukumu kifungo cha miaka 15 jela Bi. Idamange Yvonna baada ya kumkuta na hatia ya kuchochea machafuko ya umma, kukana mauaji ya kimbari na kuitisha maandamano mbele ya ikulu ya Rais Kagame.

Idamange mwenye umri wa miaka 42 alitumia mtandao wake wa Youtube akidai kuwa mtetezi wa demokrasia nchini Rwanda, alijiondoa katika kesi hiyo akisema hatarajii kupata haki kisheria.

Yeye alikanusha mashtaka hayo akisema ana uhuru wa kisheria wa kutoa maoni yake.

Mahakama ilisema kwamba bi. Idamange alikiuka na kuvuka mipaka ya sheria ya uhuru wa kutoa maoni kama inavyopendekezwa na katiba na kama alivyodai mwenyewe wakati alipohojiwa na idara ya upelelezi na mwendesha mashtaka.

Mahakama imekubaliana na mwendesha mashtaka kuhusu msingi wa mashtaka dhidi ya Idamange kwamba kupitia mtandao wake wa Youtube amekuwa akirusha vipindi vya kuchafua sura ya serikali ya Rwanda na kuhamasisha wananchi kutokuwa na imani na utawala uliopo.

Jaji ametangaza hukumu ya kifungo cha miaka 15 gerezani na faini ya franga milioni mbili sawa na dolla 2,000 dhidi ya Idamange aliyedai kuwa mwanaharakati wa demokrasia nchini Rwanda.

Bi idamange aliyekamatwa mwezi Februari mwaka huu na kuzuliwa katika gereza la Mageragere aligoma kufika mahakamani wala kesi yake kusikilizwa kwa njia ya video na mwishowe kukataa jaji aliyeendesha kesi dhidi yake ambaye hata hivyo alirejeshwa na mahakama na kuendelea kusimamia kesi hiyo.

Chanzo: BBC Swahili