Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaharakati mashuhuli Tunisia akamatwa na polisi

Polisi Tunisia Mwanaharakati.jpeg Mwanaharakati mashuhuli Tunisia akamatwa na polisi

Sun, 12 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi wa Tunisia wamemkamata mwanaharakati wa kisiasa, Khayam Turki na kumpeleka kusikojulikana. Hayo yameelezwa na wakili wake Abdelaziz Essid.

Turki, mwenye umri wa miaka 58, aliwahi kuzingatiwa kama mgombea angeliweza kuiongoza serikali baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Elyes Fakhfakh mnamo mwaka 2020, na ni mwanachama wa chama cha demokrasia ya kijamii cha Ettakatol.

Tunisia imeshuhudia ongezeko la kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa wanasiasa, waandishi wa habari na watu wengine tangu Rais Kais Saied kutwaa mamlaka muhimu katika hatua kali dhidi ya bunge mnamo Julai mwaka 2021. Tangu wakati huo, wapinzani wa Saied wamemtuhumu kwa ubabe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live