Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaharakati aliyetekwa nyara Bob Njagi yuko hai - Rais wa wanasheria

Mwanaharakati Aliyetekwa Nyara Bob Njagi Yuko Hai   Rais Wa Wanasheria.png Mwanaharakati aliyetekwa nyara Bob Njagi yuko hai - Rais wa wanasheria

Fri, 20 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Mwanaharakati Bob Micheni Njagi na ndugu Jamil na Aslam Longton, ambao walikuwa wamebatizwa jina la Kitengela Watatu baada ya kutekwa nyara mwezi mmoja uliopita katika mji wa Kaunti ya Kajiado, wako hai.

Watatu hao walisema waliachiliwa alfajiri ya Ijumaa, Septemba 20, saa chache baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kuapishwa.

Ndugu hao wa Longton walisema waliachiliwa na waliowateka na kuahidi kutoa taarifa zaidi kupitia kwa rais wa Chama cha Wanasheria nchini (LSK) Faith Odhiambo.

Video iliyotumwa kwenye ukurasa wa X na Bi Odhiambo ilionesha kuwa ndugu hao wa Langton waliachiliwa mahali fulani huko Gachie na wakatembea hadi kwenye nyumba ambapo walidaiwa kuchaji simu zao za mkononi kabla ya kumpigia simu rais wa LSK.

"Mnamo saa moja asubuhi Bob Njagi alifanikiwa kutafuta njia hadi kituo cha polisi cha Tigoni na kupata usaidizi. Yuko hai," Bi Odhiambo alisema.

"Kwa familia, marafiki na kila Mkenya ambaye ameendelea kuniombea, napenda kuthibitisha kuwa mimi ni mzima na pamoja na familia yangu. Sasa ni wakati wa kunyamazisha kelele, kushukuru kwa maisha na kila mtu atafakari kwa nini Kenya.

Watatu hao waliotekwa nyara mnamo Agosti 19 huko Kitengela, waliachiliwa muda mfupi kabla ya Naibu Inspekta Jenerali Gilbert Masengeli kuashiria kwamba angefika kortini kuomba msamaha mahakamani na kueleza waliko.

Bw.Masengeli alipatikana na hatia ya kudharau mahakama na Jaji Lawrence Mugambi na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Chanzo: Bbc