Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaharakati ahukumiwa kwenda jela miaka 6

Loujain Alhathloul 660x400 Mwanaharakati ahukumiwa kwenda jela miaka 6

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Mahakama moja nchini Saudi Arabia imemhukumu mwanamke mwanaharakati wa haki za binadamu, Loujain al-Hathloul kutumikia kifungo cha miaka sita.

Chombo cha habari cha Sabq chenye uhusiano na serikali kimesema mahakama ya kupambana na ugaidi ya Saudi Arabia imemkuta al-Hathloul na hatia ya uchochezi wa kuleta mabadiliko, akifuata ajenda ya kigeni na kutumia mtandao wa intaneti kuharibu utulivu wa umma.

Al-Hathloul amekuwa jela tangu mwaka 2018 baada ya kukamatwa pamoja na wanawake wengine raia wa Saudi Arabia zaidi ya 12 ambao ni wanaharakati wa haki za binadamu.

Alikuwa akishinikiza kuwepo mageuzi kama vile sheria ya mwanaume kumsimamia mwanamke na kuwaruhusu wanawake haki yao ya kuendesha magari.

Kesi ya mwanamke huyu imekosolewa na wataalam wa haki za binadamu wa UN, makundi ya haki za binadamu na wabunge wa Marekani na Umoja wa Ulaya.

“MIGUU KUVIMBA KAMA MBIVU, POMBE NI DAWA IKIZIDI FIGO INAFELI”

Chanzo: millardayo.com