Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaharakati Diane kuchuana na Kagame urais wa Rwanda

Diane Shima Rwigara Kagame.jpeg Diane Shima Rwigara na Kagame.

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasiasa kutoka kambi ya Upinzani Diane Shima Rwigara ametangaza kuwania Urais katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.

Kupitia mtandao wa X ambao zamani ulikuwa unaitwa Twitter ameandika kuwa “historia mpya na alama kubwa kwa Rwanda, sote kwa pamoja tutaweka historia”.

Katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 2017 Bi.Diane Shima Rwigara alipigwa chini kuwania kiti cha Urais baada ya tume huru ya uchaguzi kusema kuwa alikuwa hakidhi vigezo na kumuondoa kwenye orodha ya wagombea.

Diane Rwigara atachuana na Rais Paul Kagame ambaye aliteuliwa na chama kilichopo Madarakani cha Rwandan Patriotic Front (RPF) kukiwakilisha katika uchaguzi wa mwezi Julai 15, 2024, Rais Paul Kagame ikiwa ni muhula wake wa nne kukaa madarakani.

Kagame alishinda uchaguzi ambao muhula wake ulikuwa ni miaka saba uliofanyika mara ya mwisho Agosti 2017 kwa kupata asilimia 98.63 ya kura, kulingana na tume ya uchaguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live