Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanahabari wa zamani Richard Chacha afurahia baada ya bintiye kupata alama ya A

Ce50d6f70d457222 Mwanahabari wa zamani Richard Chacha afurahia baada ya bintiye kupata alama ya A

Tue, 11 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Bintiye Richard Chacha ni miongoni mwa maelfu ya watahiniwa waliofanya mtihani wa KCSE mwaka 2020

- Chacha kupitia mitandao ya kijamii amempongeza bintiye kwa kupata gredi ya A- kwenye mtihani huo

- Mtahiniwa Simiyu Robinson Wanjala wa Shule ya Upili ya Murang'a ndiye aliyeibuka mshindi kwa kupata maksi 87.334 kote nchini

Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya NTV na sasa Mkurugenzi wa mawasilano katika kaunti ya Mombasa Richard Chacha anasherehekea ushindi wa bintiye katika mtihani wa KCSE.

Stacy Chacha alikuwa miongoni mwa watahiniwa waliofanya bora zaidi katika mtihani wa kitaifa wa mwaka wa 2020 licha ya kukubwa na janga la ugonjwa wa corona.

Kulingana na ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter, Chacha alifichua kwamba bintiye akiweza kujizolea gredi ya A-, matokeo ambayo yamemfurahisha pamoja na familia yake.

" Hongera Stacy Chacha kwa kupata alama ya A-, umenifanya nifurahi sana pamoja na familia yangu," Chacha aliandika Facebook.

Mashabiki wake pia mitandaoni hawangeweza kuficha furaha yao na waliweza kutuma jumbe zao za pongezi.

Habari hizi njema zinajiri wiki chache baada ya Chacha kupakia picha mitandaoni akiwa na Stacy akimtakia kila la heri katika mtihani wake wa kitaifa.

Chacha alipata ajali mwaka wa 2012 ambapo alipooza baadhi ya sehemu ya mwili wake lakini amezidi kuchapa kazi licha ya hali yake ya kiafya.

Viongozi wengine waliosherehekea ushindi wa wana wao ni pamoja na seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale na aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko.

Kupitia mitandao ya kijamii Jumatatu , Mei 10, Khalwale alimpea kongole mwanawe Engine Kukaste kwa kuibuka miongoni mwa watahiniwa bora nchini.

Khalwale alisema Kukaste ambaye alikuwa akisoma katika shule ya upili ya Alliance alipata gredi ya B+ katika mtihani wa kitaifa mwaka wa 2020.

Aidha, Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko naye alimsherehekea mwanawe wa kupanga Gift Osinya kwa kupata alama ya B-.

" Baada ya kupata alama ya 399 katika mtihani wa KCPE, Gift Osinya alijiunga na shule ya upili ya Lenana ambapo pia ametufurahisha miaka minne baada ya kupata gredi ya B- katika mtihani wake wa kitaifa wa KCSE," Sonko alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke