Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanahabari Seth Olale ampoteza mwanawe, aandika ujumbe wa kuhuzunisha

0fgjhs7unr0g5o0vb Mwanahabari Seth Olale ampoteza mwanawe, aandika ujumbe wa kuhuzunisha

Sat, 10 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mwanahabari wa runinga ya NTV Seth Olale pamoja na familia yake wanaomboleza kufuatia kifo cha mtoto wao wa miaka mitatu, Myles Moses.

Olale alitangaza kifo cha mtoto Myles kupitia kwenye mitandao ya kijamii, Jumamosi , Aprili 10, hata hivyo hakutaja marehemu alikuwa akiugua ugonjwa upi.

Aidha, Olale amemtakia dua njema mwanawe na kumshukuru Mola kwa miaka mitatu ambayo aliwabariki na malaika huyo.

Myles alifariki dunia Ijumaa, Aprili 9, akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi, TUKO.co.ke ilifahamishwa.

"Tutaendelea kukuonyesha mapenzi ya dhati. Asante kwa miaka mitatu na miezi nne tulioweza kukuwa na wewe, ipo siku tutajumuika tena kwa upendo na furaha. Kwaheri ya kuonana baba tunakupenda." Aliandika Seth Olale

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke