Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi wa Zambia aliyefariki nchini Ukraine alikuwa akipigana kundi la Wagner

Dbfbf0f3 469f 4e7a B511 110dd35a5095 Mwanafunzi wa Zambia aliyefariki nchini Ukraine alikuwa akipigana kundi la Wagner

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Mfanyabiashara wa Urusi Yevgeny Prigozhin, na mshirika wa karibu wa Rais Vladimir Putin, Jumanne alisema mwanafunzi wa Zambia aliyefariki nchini Ukraine alikuwa akipigania Kundi lake la Kijeshi la Wagner.

Zambia ilisema inahitaji kupata taarifa kutoka Moscow na ipewe maelezo ya jinsi Lemekhani Nyirenda, 23, alivyotoka kutumikia kifungo karibu na mji mkuu wa Urusi hadi kufa vitani mwezi Septemba.

Katika kujibu maswali, wizara ya mambo ya nje ya Zambia na ushirikiano wa kimataifa ilisema "imejishughulisha kwa dhati" katika kujaribu kurejesha mwili wa kijana huyo.

Babake Nyirenda alisema alikuwa akitumikia kifungo cha miaka tisa jela nje kidogo ya jiji la Moscow kwa kosa la kutumia dawa za kulevya wakati "alipoandikishwa" kupigana.

Familia yake ilisema haikuwa wazi jinsi alivyoajiriwa au na nani.

Siku ya Jumanne, kundi la Prigozhin lilisema Nyirenda alikuwa ameajiriwa na Wagner.

Kumekua na madaia kuwa Prigozhin na wawakilishi wengine wa Wagner wamezuru magereza ya Urusi yanayotoa msamaha kwa wahalifu kujisajili kupigania Urusi nchini Ukraine.

"Ndiyo, namkumbuka vizuri mtu huyu," Prigozhin alisema katika jibu la maandishi kwa swali kutoka kwa mwandishi wa habari kama Mzambia huyo alikuwa akimpigania Wagner.

Prigozhin alisema Nyirenda alikufa kama "shujaa" na kwamba alikuwa "mmoja wa watu wa kwanza kuingia kwenye mahandaki ya adui mnamo Septemba 22".

Shirika la habari la Reuters linasema halikuweza kuthibitisha mazingira ya kifo cha Nyirenda au madai ya Prigozhin kwamba alijiunga na Wagner kwa hiari.

Kwa kuwa kwa miaka mingi alikataa uhusiano wake na Wagner na kufanya kazi katika vivuli, Prigozhin katika miezi ya hivi karibuni amepitisha uwepo wa uthubutu zaidi kwenye eneo la ndani la Urusi, akikosoa uongozi wa kijeshi, akikiri kwamba ndiye aliyeanzisha Wagner na kukubali kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Chanzo: Bbc