Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chuka ajiua kwa kujirusha kutoka orofa ya sita

4091dea925f6af83 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chuka ajiua kwa kujirusha kutoka orofa ya sita

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Japo haijabainika wazi chanzo cha mrembo huyo kujitoa uhai, inasemekana kuwa alikuwa ametofautiana na mpenzi wakeKulingana na mashahidi, marehemu ambaye anadaiwa alikuwa mjamzito, alimtuhumu mpenzi wake kuwa mzinziMwanafunzi huyo alithibitishwa kufariki alipowasili hospitalini kutokana na majeraha mabaya aliyopata

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chuka katika kaunti ya Tharaka Nithi, alijitoa uhai baada ya kujirusha kutoka orofa ya sita ya jengo la chuo hicho siku ya Jumapili Juni 27 jioni.

Mwanafunzi huyo anaripotiwa kujirusha kutoka kwa jengo la Science Complex la chuo hicho.

Japo haijabainika wazi chanzo cha mrembo huyo kujitoa uhai, inasemekana kuwa alikuwa ametofautiana na mpenzi wake.

Kulingana na mashahidi, marehemu ambaye anadaiwa alikuwa mjamzito, alimtuhumu mpenzi wake kwa uzinzi.

Maafisa wa kutoa idara dharura walikimbia katika eneo la tukio na kumkimbiza katika hospitali iliyoko karibu baada ya kumfanyia huduma ya kwanza lakini alithibitishwa kufariki alipowasili.

Kufikia sasa bado uongozi wa chuo hicho haujatoa taarifa kuhusu tukio hilo.

Ingawa maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi huku mashahidi wakiandikisha taarifa.

Kwingineko Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Yanyonge eneo la Mwingi ya Kati kaunti ya Kitui Kioko Mutie alijitoa uhai kwa kujinyonga ndani ya ofisi yake.

Kisa hicho ambacho kilitokea siku ya Jumatatu, Juni 21, kiliwashangaza na washtua walimu pamoja na wazazi ambao walimtaja kuwa mwalimu mchapakazi na msikiivu kwa wanafunzi.

Kioko hakuwacha ujumbe wowote wa kuashiria kiini cha yeye kujinyonga. Akithibitisha kisa hicho, Chifu msaidizi wa kaunti ya Kitui Mulinge Wambua alisema kwamba mwalimu huyo wa miaka 46 alikuwa mchangamfu na hakuwahi onyesha dalili za kuwa na msongo wa mawazo.

Walimu wenzake walisema alipenda taaluma yake na angefika shuleni mapema hata kama sio wiki ambalo hayupo kwenye zamu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke