Mwanafunzi wa Kemia ya Biolojia katika Chuo Kikuu cha Port Harcourt (UNIPORT), Otuene Justina Nkang, amepatikana amefariki katika nyumba ya mpenziwe katika mji mkuu wa Jimbo la River State.
Nkang alikuwa ameripotiwa kutoweka kwa siku nne baada ya kuondoka kazini, alikokuwa akifanya mafunzo ya viwandani katika hospitali ya kibinafsi huko Port Harcourt.
Kama ilivyoripotiwa na Daily Trust, chanzo kilisema mpenzi wa Nkang alimuua na kumkatakata sehemu za mwili wake.
Marehemu alisemekana kuwa alimtembelea mpenziwe katika eneo la nyanda za juu huko Port Harcourt.
Duru hizo zilisema maafisa wa usalama katika eneo hilo lilimkamata mshukiwa huyo wakati wakijaribu kuitupa maiti iliyokuwa ikioza kwenye jaa la taka.
Kulingana na Vanguard, mshukiwa, Collins, alikamatwa baada ya maafisa wake wa usalama wa mali kugundua sehemu za mwili wa Justina zilizokatwa kwenye magunia yenye damu.
Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha, Ofisa Mahusiano wa Umma, SP Grace Iringe Koko, alisema kuwa Kamishna wa Polisi, Policarp Emeka Nwaonyi, atazungumza na wanahabari kuhusu suala hilo.
Kwingineko, wingu la huzuni lilitanda chuo kikuu cha Pwani kufuatia kifo cha mwanafunzi.
Faith Adongo Owino alifariki dunia kufuatia shambulizi linaloshukiwa kuwa la kisu mwendo wa saa 7:30 usiku Ijumaa, Oktoba 20.
Inasemekana kwamba Faith alidungwa kisu mara kadhaa na washambuliaji wake kwenye barabara inayojulikana sasa hivi ya Misufuni alipokuwa akirejea nyumbani.
Alikimbizwa katika kitengo cha dharura cha Hospitali ya Wilaya ya Kilifi, ambapo aliaga dunia mwendo wa saa nne usiku.
Kulingana ujumbe wa mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Pwani, Nashon Okoth ambaye aliomba msaa da wa damu, Faith alivuja damu kupita kiasi.
"Masalkheri ndugu zanguni. Hii ni kufuatia kesi ya mwenzetu ambaye alidungwa kisu. Tunatoa wito kwa yeyote aliye na damu aina ya A+ kufika katika wodi ya dharura katika hospitali ya Wilaya ya Kilifi ili tuweze kuokoa maisha yake," ujumbe huo ulisema.