Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi darasa sita ajinyonga kwa kutumia shuka

Kujinyonga?fit=800%2C445 Mwanafunzi darasa sita ajinyonga kwa kutumia shuka

Fri, 5 Aug 2022 Chanzo: Radio Jambo

Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha msichana mwenye umri wa miaka 13 ambaye anaripotiwa kufariki kwa kujitoa mhanga katika nyumba ya familia yao iliyoko Kibera, Nairobi.

Mwanafunzi wa darasa la sita anasemekana alitumia shuka kujitoa uhai siku ya Jumanne.

Kulingana na polisi, mtoto huyo alifunga shuka kwenye paa ili kujinyonga. Mwili wake ulipatikana ukining’inia kutoka kwa paa mamake alipoenda kumwamsha baada ya kungundua kuwa amelala kwa muda.

Kesi mbili sawia za kujitoa mhanga huko Pangani na Buruburu pia ziliripotiwa kwa polisi Jumanne. Wahasiriwa ni pamoja na mwanamke aliyekufa alijinyonga.

Visa vya watu kujiua vimeongezeka mwaka huu na viongozi wanalaumu hali hiyo kuwa ni msongo wa mawazo.

Kwani maeneo mbalimbali vimeripotiwa kuadhirika sana kwa idadi ya vifo zikiwemo, Eregi, Kakamega, ambapo mwanume anayejulikana kama James Lirubi, 55, alifariki kwa kujinyonga nyumbani kwake huku katika eneo la Matungu, Vivian Warire mwenye umri wa miaka 21 akifariki kwa kujitoa uhai nyumbani kwake. Alikuwa mjamzito.

Kwingineko kulingana na polisi, mwanafunzi wa udaktari alifariki kwa kujinyonga katika chumba chake eneo la Nzambani, Seku, Kaunti ya Kitui. Mwili wa Brian Kipkoech ulipatikana katika chumba chake muda mrefu baada ya tukio hilo kutokea.

Na katika eneo la Sultan Hamud, Kaunti ya Makueni, mwili wa Philip Mutuku, 39, ulipatikana ukining’inia juu ya mti.

Chanzo: Radio Jambo