Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi auawa kwenye vurugu Kenya

Rais Wa Kenya Asema Hakuna Mtu Aliye Juu Ya Sheria Mwanafunzi auawa kwenye vurugu Kenya

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafunzi mmoja auawa nchini Kenya siku ya Jumatatu, wakati makabiliano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji wanaoipinga serikali yakipamba moto, baada ya kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga kuitisha maandamano ya kila wiki, kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha.

Polisi wa kutuliza ghasia walirusha mabomu ya machozi na maji ya kuwasha, dhidi ya waandamanaji na msafara wa Odinga, huku mapigano yakizuka kati ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe na polisi, katika sehemu za mji mkuu Nairobi na angalau mji mwingine mmoja.

Viongozi wakuu wa upinzani, pia walikuwa miongoni mwa watu kadhaa waliokamatwa.

Polisi wamesema mwanafunzi wa chuo Mwaka wa tatu William Mayange, aliuawa kwa kujeruhiwa shingoni baada ya maafisa kufyatua risasi za moto, wakati wa mapigano na waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live