Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi auawa kwa kupigwa risasi Afrika Kusini

Mwanafunzi Auawa Kwa Kupigwa Risasi Afrika Kusini Mwanafunzi auawa kwa kupigwa risasi Afrika Kusini

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mwanafunzi wa chuo kikuu ameuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya kwa risasi kwenye barabara yenye shughuli nyingi karibu na katikati mwa jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini, polisi wamesema.

Wanafunzi hao walipigwa risasi wakati basi lao lilipokuwa likipita eneo ambalo watu wenye silaha walikuwa wakiwapiga risasi wanaume wawili waliokuwa kwenye gari lililokuwa limeegeshwa.

Hakuna aliyekamatwa hadi sasa.

"Wanaume wawili waliokuwa kwenye gari na mwanafunzi mmoja walitangazwa kufariki huku mwanafunzi mwingine akipelekwa katika hospitali ya karibu kwa matibabu," msemaji wa polisi Kanali Dimakatso Nevhuhulwi aliambia BBC.

Taarifa ya polisi ilisema wanafunzi hao walijikuta katikati ya ufyatulianaji risasi.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mwili wa mwanaume ukining'inia kwenye dirisha la gari. Nyingine inaonyesha kile kinachoonekana kama mtu anayetibiwa kwenye eneo la tukio kwenye barabara kuu ya Braamfontein.

Chuo Kikuu cha Johannesburg kilisema wanafunzi wote wawili walioathirika walikuwa wanasoma katika chuo hicho.

Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ambaye aliuawa alikuwa na umri wa miaka 18 na alikuwa akisafiri kurudi kwenye makazi yake alipopigwa risasi, chuo kikuu kilisema.

Msemaji wa polisi wa jiji la Johannesburg, Xolani Fihla alisema chanzo cha ufyatuaji risasi hakijajulikana.

Kati ya Julai na Septemba mwaka jana wastani wa watu 34 waliuawa kwa kupigwa risasi kila siku nchini Afrika Kusini, takwimu za uhalifu za polisi zinasema.

Chanzo: Bbc