Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi anaswa na misokoto 16 ya bangi bwenini

Bangi Mwanafunzii Mwanafunzi anaswa na misokoto 16 ya bangi bwenini

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi katika Kaunti ya Migori wanamzuilia mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari baada ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi shuleni.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 alinaswa akiwa na misokoto 16 ya bangi wakati wa ukaguzi wa bweni uliofanywa katika shule hiyo iliyo eneo la Ntimaru siku ya Jumatatu.

Wasimamizi wa shule pia walikuta mshukiwa akiwa ameficha kiberiti kimoja cha vijiti, kiberiti cha gesi na karatasi mbili za kufungia sigara.

Polisi wameripoti kuwa mshukiwa alikamatwa baada ya wasimamizi wa shule kutoa ripoti kuhusu yaliyojiri.

"Hili linapaswa kutoa onyo kwa wanafunzi wote kuepuka njia ya uhalifu kupitia matumizi mabaya ya dawa za kulevya na aina nyinginezo za uhalifu. Utumiaji wa madawa ya kulevya hauna faida katika maisha, husababisha tu uharibifu," Tume ya Huduma kwa Polisi (NPS) ilionya katika taarifa yake ya Jumanne.

NPS ililaani vikali matumizi ya dawa za kulevya shuleni huku ikiwataka wanafunzi wote kujiepusha nazo na badala yake kutia bidii masomoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live