Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi aliyekuwa ametekwa aachiwa huru

Diana Chepkemoi.jpeg Mwanafunzi aliyekuwa ametekwa aachiwa huru

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa amesema Diana Chepkemoi, ambaye alikuwa amezuiliwa ndani kinyume na matakwa yake huko Riyadh, ameachiwa baada ya juhudi za viongozi na baadhi ya raia wa Kenya.

Aida ameongeza kuwa mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu ambaye alikuwa akifanya kazi za ndani amepelekwa hospitali kwaajili ya uchunguzi wa Afya yake kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Ubalozi wa Kenya mjini Riyadh umetuma maafisa wake kwa ajili ya kutembelea hospitali hiyo huku Barasa akiitaka Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje kufanya uchunguzi wa mashirika ya ajira nchini humo ili kudhibiti matukio kama hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live