Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi akamatwa na barua ya mapenzi

Barua Mapenziiiii Mapenzii.png Mwanafunzi akamatwa na barua ya mapenzi

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msichana mmoja aitwaye Shindara Maya kutoka nchini Nigeria aliibua gumzo mitandaoni baada ya kuanika barua ambayo mdogo wake wa kiume ambaye ni Mwanafunzi alikuwa amemwandikia mwanafunzi mwenzake wa kike. Akimtaja msichana huyo kama "Waridi la Sharon". 'Rose of Sharon'.

Barua hiyo aliianika kwenye mtandao wa TikTok, kupitia video inayoonyesha barua ya mapenzi ambayo mdogo wake alinaswa nayo nyumbani.

Msichana huyo alifichua kwamba mdogo wake huyo aliporudi kutoka shuleni, mama yao alimwita na kumwambia angependa kupekua begi lake.

Begi lilipofunguliwa, waligundua barua ya mapenzi aliyomwandikia Mwanafunzi mwenzake darasani.

Sehemu ya barua hiyo ilisomeka: "Nakupenda sana kwa sababu nilipokuona mara ya kwanza kwa macho yangu nilisema kimoyomoyo, 'Mungu wangu, hebu mwone mrembo huyu'.... huwa nakuwaza nyakati zote na kukupenda."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live