Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi ajishindia ruzuku ya kujenga ukumbi wa burudani Kenya

Mwanafunzi Ajishindia Ruzuku Ya Kujenga Ukumbi Wa Burudani Nchini Kenya Mwanafunzi ajishindia ruzuku ya kujenga ukumbi wa burudani nchini Kenya

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Brighton ameshinda ruzuku ya kujenga klabu ya usiku na studio ya muziki katika nchi yake ya asili ya Kenya.

Jesse Mugambi alihitimu shahada ya usanifu na sasa anasomea shahada ya uzamili ya muundo endelevu chuo kikuu cha Moulsecoomb.

Mradi huo, unaoitwa Studio Can-V, utapokea €50,000 (£39,000) kutoka kwa Jägermeister kusaidia kufadhili maeneo hayo, yaliyotengenezwa kutokana na kontena za usafirishaji jijini Nairobi.

"Baada ya kukumbana na changamoto katika kufuata ndoto yangu ya muziki, ninasukumwa na imani kwamba kuna vijana na wazee wengi wanaotamani fursa za kutimiza ndoto zao za muziki," Bw Mugambi alisema.

Mradi huo, ulioendelezwa wakati wake kama mwanafunzi wa shahada ya kwanza katika chuo kikuu, utalenga kutengeneza fursa ya kubadilisha kituo cha ma-DJ wanaoibukia nyakati za mchana na kuwa kilabu wakati wa usiku.

Studio inayohamishika itajengwa na mafundi wa ndani jijini Nairobi kutoka kwa makontena ya usafirishaji yaliyotengenezwa upya.

Kwa kutumia miundo ya kienyeji kukuza utambulisho wa kitamaduni wa vijana, Bw Mugambi alisema alitaka kuleta mabadiliko chanya kupitia muziki, densi na uhusiano.

"Studio Can-V inakuza ushirikishwaji kwa kutanguliza sauti za vijana wa DJ kutoka jamii na asili mbalimbali, ambao wanawakilisha mustakabali wa jamii sawa," alisema.

Chanzo: Bbc