Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanadada kutoka Kenya afariki Uarabuni, familia yajulishwa miezi sita baadae

Mwanakombo Bahmad Mwanadada kutoka Kenya afariki Uarabuni, familia yajulishwa miezi sita baadae

Mon, 12 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia moja katika kaunti ya Mombasa inazidi kulilia haki baada ya mpendwa wao kusemekana kufariki katika taifa la Saudi Arabia mwezi mmoja tu baada ya kutua katika taifa hilo la Uarabuni.

Kutilia msumari moto kwenye kidonda, familia hiyo inasema kwamba mwanao alifariki mwezi Februari mwaka huu ila wamekuja kujulishwa mwezi Agosti, miezi sita baadae na wanaambiwa kwamba mwili huo wa mwanao utasafirishwa nchini baada ya miezi miwili ijayo, kufanya jumla ya miezi 8 tangu kifo chake kutokea kwa sababu zisizoeleweka.

Katika ripoti ya kituo kimoja cha runinga humu nchini, Mwanakombo Bahmad mwenye umri wa miaka 23 alisafiri kutoka nchini Januari mwaka huu na ghafla mawasiliano yakapotea baina yake na familia yake.

Mamake aliambia runinga hiyo kwamba alikuja kufahamishwa miezi sita baadae kwamba mtoto wake alishafariki kitambo.

“Ni juzi hiyo mwezi wa nane tarehe kumi na nne ndio napata hizo habari, na Mwanakombo alifariki tangu mwezi wa pili tarehe tano. Sasa nikashangaa kwa nini hawakunielezea kutoka hizo siku, hiyo ndio uchungu ambayo ninahisi.

Ninahangaika mchana na usiku na sikupata hiyo salamu kama mtoto wangu amekufa,” Mishi Khamis aliambia ripota baina ya majonzi na uchungu mkali wa mama kumpoteza mwana.

Kulingana na familia hiyo, baada ya kumjulisha ajenti aliyemsafirisha mwanao Kwenda Saudi Arabia aliwapa kisogo hata baada ya kumtaarifu kwamab mwanao anasema anateswa. “Kila nilipokuwa nikimpigia ajenti simu, alikuwa ananiambia kwamba Mwanakombo alitoroka,” alieleza.

Taarifa hizi zinakuja siku chache tu baada ya mwanadada mmoja Diana Chepkemoi kuokolewa kutoka Saudia alipokuwa akifanya kazi na kuonekana kudhoofika kiafya mno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live