Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwana wa kike wa Nelson Mandela aaga dunia

Zindzi Mwana wa kike wa Nelson Mandela aaga dunia

Mon, 13 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zindzi Mandela, mwana wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela na Winnie Madikizela - Mandela, amefariki kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo SABC.

Zindzi amefariki mjini Johannesburg mapema Jumatatu akiwa na umri wa miaka 59.

Kifo chake kimethibitishwa na chanzo kimoja cha familia, kimesema chombo cha habari cha SABC.

Alikuwa balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark. Amewaacha watoto wanne na mumewe.

Mwanamke huyo alikuwa mwanarakati wa kisiasa na ni miongoni mwa wale waliopigana dhidi ya uongozi wa ubaguzi wa rangi nchini humo.

Alianza kuhudumu kama balozi wa Denmark mwaka 2015.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live