Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwambieni anitafute!: Kalonzo adokeza yuko radhi kufanya kazi na DP Ruto

Dad56ce760aa3edd Mwambieni anitafute!: Kalonzo adokeza yuko radhi kufanya kazi na DP Ruto

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kalonzo Musyoka alisema kwamba ingawa William Ruto hakuwa amemkaribisha katika meza ya mazungumzo ya kuunda muungano, yeye yuko tayari kushirikiana na DP Ruto Kalonzo alisema kwamba Ruto amekaribishwa eneo la Ukambani ili kupiga kampeni zake za urais Kiongozi huyo wa Wiper alionekana kubatilisha msimao wake ambapo awali alisema ni heri astaafu siasa kuliko kumuunga mkono RailaKiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ameonyesha ari ya kufanya kazi na Naibu Rais William Ruto.

Kalonzo alisema hata ingawa Ruto hakuwa amemualika kwenye mazungumzo ya kuunda serikali, yeye yuko tayari kushirikiana naye kwa sababu "Wakenya ni sharti washauriane."

"La, haijafikia kiwango hicho. Iwapo utasikia wakinitafuta, waambie niko kwa sababu Wakenya lazima washuriane. Iwapo watahitaji kuzungumza nami, basi wanakaribishwa," Kalonzo alisema kwenye mahojiano na jarida la Jumamosi la Nation mnamo Novemba 6.

Kalonzo alisema kwamba ingawaje Ruto amekaribishwa kuzuru maeneo ya Ukambani kupiga kampeni za kuwania kiti cha urais 2022, alidai kwamba yeye huwahonga wenyeji ili wahudhurie mikiutano yake ya siasa.

"Lakini tanapaswa tujue kwamba Wakamba ni watu waerevu sana. Anaweza kuwa pale mara 100. Watachukua pesa zake na zawadi. Mimi huwa nashangaa ni kwa nini yeye huwahonga watu wa Ukambani na wala sio Eldoret...Ila uamuzi ya ni nani atakuwa rais ni swala tofauti ambalo pesa na zawadi haziwezi kununua," Kalonzo alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke